Mbappe Aweka Rekodi Mpya Kombe la Dunia Qatar- Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mshambuliaji kutokea timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe ameibuka mshindi wa tuzo ya mfungaji bora katika mashindano ya kombe la dunia mara baada ya kumaliza mashindano hayo kwa jumla ya mabao 8 na bao moja likipatikana katika mikwaju ya Penalti.

Mbappe mwenye miaka 23 alianza kuichezea timu yake ya Taifa ya Ufaransa katika kombe la dunia lililofanyika Urusi mwaka 2018 akiwa na miaka 19 pekee.

Katika mashindano ya kombe la dunia nchini Urusi mchezaji huyo alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 4 katika mashindano hayo huku Ufaransa wakiibuka mabingwa wa kombe hilo kwa mara ya pili tangu mwaka 1998. Mbali na hayo pia baada ya mashindano hayo kuisha kinda huyo wa kipindi hicho aliondoka kama mshindi wa tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo.

Nchini Qatar bado kylian Mbappe amezidi kung'ara mara baada ya kushinda mashindano ya kombe la dunia kama mfungaji bora akiwa na jumla ya mabao 8 pamoja na pasi 2 za usaidizi wa magoli.

Licha ya kuwa ufaransa walizidiwa na Argentina lakini ndani ya muda wa dakika 2 Mchezaji huyo ambaye pia anaichezea  PSG ya Ufaransa aliinua tumaini kwa timu yake ya Taifa waliokuwa wamezidiwa nguvu na Argentina kwa kufunga mabao mawili ambapo bao la kwanza lilipatikana katika dakika ya 80 na bao la pili katika dakika ya 81 na kusawazisha mabao ya Argentina yaliyopatikana katika kipindi cha kwanza.

Mbappe alifanikiwa kuikamilisha hat-trick mara baada ya kufunga bao la tatu katika ile dakika ya 118 na kujiwekea rekodi ya kufunga mabao matatu katika fainali za kombe la dunia baada ya ile rekodi ya Geoff Hurst mwaka 1966 Uingereza walipobeba kombe la dunia baada ya kumfunga Ujerumani Magharibi.

Licha ya kushindwa kubeba kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar lakini mpaka sasa Kylian Mbappe tayari ameonesha kuwa moja kati ya wachezaji wenye uwezo mkubwa uwanjani na faida ya ufundi wake ni spidi akiwa uwanjani inayomfanya azidi kuwa tishio kwa wapinzani akiwa moja kati ya wachezaji ghali zaidi dunia.

Akiwa bado Ligue 1 mfaransa huyo tayari ana vikombe vinne vya ligi hiyo, tuzo za mfungaji bora kwa misimu minne tofauti, akiwa na Ufaransa tayari Mbappe ameweza kunyakua ubingwa wa dunia, Ubingwa wa Mataifa Ulaya, mchezaji bora mwenye umri mdogo Katika mashindano ya kombe la dunia nchini Urusi, pamoja mfungaji bora wa kombe la dunia 2022 huko Qatar na kazi bado inaendelea.

Leave your comment

Top stories