Benzema Athibitisha Kuachana Na Ufaransa- Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema, amethibitisha kuachana na timu yake ya Taifa masaa machache mara baada ya timu hiyo kushindwa kutetea ubingwa wao katika kombe la dunia nchini Qatar.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Karim aliandika ya kuwa "Nimefanya juhudi na makosa ambayo yamepekekea niwe hapa nilipo leo na najivunia! Nimeandika historia na ya kwetu anafikia ukingoni". Ujumbe huu aliuambatanisha pamoja na picha yake akiwa amevaa jezi ya Ufaransa siku ya Jumatatu ikiwa pia ni siku yake ya kuzaliwa.

Mchezaji huyo aliyetimiza miaka 35 siku ya jumatatu siku moja mara baada ya kombe la dunia kufikia kikomo alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotakiwa kuwepo katika kikosi cha Ufaransa wakati wa mashindano ya kombe la dunia nchini Qatar lakini alishindwa kushiriki mara baada ya kupata majeraha kabla ya mechi za kombe la dunia kuanza kutimua vumbi.

Mwaka 2018 Benzema hakufanikiwa kutwaa kombe la dunia na Ufaransa mara baada ya kutokuchaguliwa kama miongoni ya wachezaji na kocha wa timu hiyo Didier Deschamps.

Akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d'or mwaka 2022 amefanikiwa kushiriki jumla ya michezo 97 na kufunga mabao 37.

Leave your comment

Top stories