Argentina Washinda Kombe la Dunia katika Fainali na Timu Ya Ufaransa- Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Hatimaye baada ya miaka 36 Argentina wameweza kuibuka mabingwa wa kombe la dunia mara baada ya kuwafunga Ufaransa kwa kikwaju ya penalti 4-2 fainali zilizochezwa katika uwanja wa Lusail.

Katika mchezo huo nyota wa soka Lionel Messi ameweza kuinua kikombe hicho kwa mara ya kwanza na kufanya aweze kumaliza kombe hilo na jumla ya mabao 8 katika mashindano hayo na pia mabao 94 katika timu yake ya Taifa.

Haukua mchezo mrahisi kwa Ufaransa haswa katika kipindi cha kwanza baada ya Argentina kutangulia kupata mabao mawili kupitia kwa Lionel Messi dakika ya 23 pamoja na Angel di Maria katika ile dakika ya 36.

Katika kipindi cha pili mara baada ya kocha Dider Deschamps kufanya mabadiliko na kumuingiza Coman Ufaransa walianza kupata matumaini na kutengeneza nafasi zaidi na kumfanya Kylian Mbape kusawazisha katika dakika ya 80 kwa penalti pamoja na ile dakika ya 81.

Dakika 90 zikakamilika na timu zote mbili zikalazimika kuingia katika dakika za nyongeza na kufanikiwa kuongeza magoli kwa pande zote mbili ambapo Argentina kupitia kwa Lionel Messi tena akafanikiwa kuongeza bao la tatu na kabla ya dakika hizo za nyongeza kutamatika Mbappe akafanikiwa kusawazisha kupitia Penalti na kuwafanya waingie katika hatua za matuta.

Kipa wa Argentina Emiliano Martinez ameonekana kuwa ndiye mlinda mlango bora zaidi katika mashindano hayo ya kombe la dunia mara baada ya kufanikiwa kuokoa jahazi la timu hiyo ya Taifa baada ya kuokoa mikwaju miwili ya Penalti na kumfanya Hugo Lloris kushindwa kuonesha uwezo wake katika penalti baada ya kuruhusu mikwaju miwili ya penalti kuzama katika nyavu za Ufaransa.

Lionel Scaloni naye pia akiwa ndiye kocha mwenye umri mdogo Katika mashindano hayo amefanikiwa kuongoza kikosi hicho cha Argentina akiwa na miaka 44 pekee.

Huu ni ushindi ambao unawafanya Argentina kuinua kombe la dunia na kulipeleka nchini humo tangu mwaka 1986.

Leave your comment