Wachezaji Walioondoka Na Tuzo Mbalimbali Kombe La Dunia Qatar-Mdundo Alt

[Picha:Sports Mole]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika huko Qatar yametamatika na Argentina wamefanikiwa kuiandika historia mara baada ya kubeba kikombe cha tatu cha dunia kwa kumfunga Ufaransa ambaye ni bingwa mtetezi wa mashindano hayo kwa mikwaju ya penalti. Wafuatao ni wachezaji mbalimbali waliofanikiwa kuondoka na tuzo mbalimbali katika mashindano hayo.

Mchezaji Bora Wa Mashindano

Lionel Messi hajaondoka na kombe la dunia pekee mara baada ya kuondoka pia na tuzo ya mchezaji bora wa mashindano hayo. Mshambuliaji huyo ambaye ametangaza kustaafu kushiriki mashindano hayo ameweza kuwa mchezaji bora wa mechi mbalimbali za michuano hiyo mara nne.

Mfungaji Bora Wa Mashindano

Akiwa na miaka 23 pekee Kylian Mbappe ameweza kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo mara baada ya kufunga jumla ya mabao 9 na kutengeneza pasi 2 za usaidizi wa magoli katika mashindano hayo.

Mlinda Mlango Bora Wa Mashindano

Kipa kutokea Argentina Emiliano Martinez ameondoka na Golden Gloves kutokana na uwezo wake uwanjani pamoja na uokoaji wake wa mikwaju ya Penalti Katika mechi mbalimbali za michuano hiyo kama vile mechi ya Argentina dhidi ya Croatia pamoja na penalti za fainali za kombe la dunia na kuifanya Argentina kuwa washindi wa michuano hiyo.

Mchezaji Bora Mwenye Umri Mdogo Katika Mashindano

Kutokea Argentina Enzo Fernandez mwenye miaka 21 ndiye ameondoka kama mchezaji bora mwenye umri mdogo akiwa amecheza jumla ya michezo saba na Argentina na kufanikiwa kufunga goli moja pamoja na pasi moja ya usaidizi wa goli katika mashindano hayo ya kombe la  dunia nchini Qatar.

Leave your comment