Makocha Waliofunga Virago Baada Ya Kuondolewa katika Kombe la Dunia- Mdundo Alt

[Picha:Click Oralando & Ghana Web]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Wakati kombe la dunia likiendelea huko Qatar tayari kuna vijimambo ambavyo vimeleta upekee wa mashindano hayo.Ukiachana na panda shuka za michuano hiyo wafuatayo ni makocha waliofunga virago vyao katika michuano ya kombe la dunia huko Qatar.

Ota Addo  (Ghana)

Si muda mrefu tangu ajiunge na Ghana mnamo mwezi wa Februari lakini mwalimu huyo wa kikosi cha timu hiyo alilazimika kuachana na timu hiyo ya taifa mara baada tu ya kuondolewa katika mashindano hayo ya kombe la dunia. Kwa mujibu wa Ado ni sababu za kifamilia ndizo zilizomlazimu kuachana na kikosi hicho cha Ghana.

Adenor Leonardo Bacchi (Brazil)

Baada ya maumivu ya kuaga mashindano ya kombe la dunia katika hatua ya robo fainali Meneja wa Brazil ambaye pia anajulikana kama Tile amemwaga manyanga katika timu ya Taifa ya Brazil licha ya kutoa taarifa mapema ya kuwa baada ya mashindano hayo angeondoka lakini imekuwa ghafla sana baada ya kipigo kutoka kwa Croatia

Louis Van Gaal (Uholanzi)

Kocha aliyekuwa akikinoa kikosi cha Uholanzi Louis Van Gaal ameamuua kuagana na timu hiyo mara baada tu ya kuondolewa katika mashindano ya  kombe la dunia na timu ya Taifa ya Argentina kwa mikwaju ya penalti. Kocha huyo aliweza kusaidia kikosi hicho cha Uholanzi kufikia hatua ya nusu fainali katika kombe la dunia mwaka 2014 bila ya mafanikio ya kuingia fainali.

Roberto Martinez (Ubelgiji)

Moja kati ya mambo yaliyoshangaza mashindano ya kombe la dunia ni baada ya kushuhudia Ubelgiji ikitolewa katika hatua ya makundi na kushindwa kufudhu hatua inayofuata. Hii yote ni baada ya timu hiyo ya taifa inayoshikilia nafasi ya pili katika viwango vya FIFA kuaga mashindano hayo. Kwa upande wa mwalimu ya timu hiyo mara baada ya timu hiyo kuaga mashindano na yeye hakuchukua muda na kuamua kuondoka katika kikosi hicho ambacho alikisaidia kufikia hatua ya robo fainali katika mashindano ya Euro 2020.

Luis Enrique (Uhispania)

Mara baada ya kuondolewa na Morocco katika hatua ya 16 bora kombe la dunia, Shirikisho la soka la nchini Uhispania lilitoa taarifa ya kuachana na mwalimu huyo na kikosi hicho cha timu ya Taifa. Baada ya taarifa hizo Kocha huyo alitumia mitandao ya kijamii na kushukuru watendaji wote pamoja na wachezaji wa timu hiyo. Luis Enrique alikisaidia kikosi cha Uhispania kufikia hatua ya nusu fainali mashindano ya Euro 2020.

 

Leave your comment

Top stories