Wachezaji Watakaoachana na Timu za Taifa Baada ya Kombe la Dunia Qatar
14 December 2022
[Picha:Instagram]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Kwa takribani miongo miwili wapenzi wa soka wameweza kushuhudia kabumbu la kipekee likisakatwa uwanjani na upinzani mkubwa baina ya wachezaji bora zaidi duniani ukionekana kutokana na viwango vya wachezaji hao. Kwa sasa mbio hizo zimeonekana zikifikia ukingoni mara baada ya mastaa hao wa soka kuachana na maisha ya kusakata kabumbu na haswa kombe la dunia mara baada ya mashindano hayo kutamatika huko Qatar. Wafuatao ni baadhi ya wanasoka hao wanaotarajia kustaafu mara baada ya kombe la dunia kutamatika huko Qatar.
Karim Benzema
Licha ya kuwa hakujiunga na kikosi ya Ufaransa katika kombe la dunia huko Qatar, mshindi huyu wa tuzo za Ballon D’or ilitarajiwa hili kuwa ndilo kombe lake la dunia la mwisho kushiriki lakini ilishindikana kutokana na majeraha kabla ya kuwasili Qatar na kufanya abwagwe na kikosi hicho cha Ufaransa na kumfanya ashindwa kushiriki.
Lionel Messi
Wakati akiwa nchini Argentina alipata wasaa wa kufanya mahojiano na kituo cha habari cha FOX News Argentina na kutamka ya kuwa hili ndilo kombe lake lake la dunia kushiriki mara baada ya kuwajibikia mashindano hayo kwa misimu mitano bila ya mafanikio akiwa na Argentina.
Eden Harzad
Nyota kutokea Real Madrid na timu ya taifa ya Ubelgiji mara baada ya kuyaaga mashindano ya kombe ya dunia huko Qatar katika hatua ya makundi muda mchache baadaye alitoa taarifa za kustaafu hivyo Qatar ndiyo safari yake ya mwisho dhidi ya mashindano ya kombe la dunia.
Luka Modric
Nahodha wa timu ya taifa ya Croatia ambaye pia ni kiungo katika timu ya Real Madrid Luka Modric atayaaga mashindano hayo ya kombe la dunia mara baada ya umri kusogea licha ya kuwa amekuwa mfano bora katika timu hiyo mara baada ya kuisaidia timu yake ya Taifa kufika fainal za kombe la dunia huko Russia mwaka 2018 bila mafanikio walipokutana na Ufaransa.
Luis Suarez
Nyota wa soka kutokea nchini Uruguai naye ameitimu safari yake ya kushiriki mashindano yya kombe la dunia mara baada ya kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho nchini Qatar katika hatua ya makundi. Safari yake inaweza isiwe nzuri kwa mashabiki wa timu ya Taifa ya Ghana baada ya tukio la mwaka 2010 katika kombe la dunia lakini haina budi kwa yeye kupumzika katika kusakata kabumbu.
Cristiano Ronaldo
Mshindi huyu wa tuzo tano za Ballon D’or ambaye kwa sasa anapitia wakati usio wa kawaida baada ya sakata lake na Manchester United huenda akaacha na kucheza mpira wa miguu katika timu ya Taifa kutokana na umri na pia alishawahi kusema endapo akifanikiwa kushinda kombe la dunia huko Qatar basi yeye na kucheza mchezo huo itakuwa ndio mwisho ambacho ni kitu kilichishindikana mara baada ya kutolewa na Morocco katika hatua ya robo fainali nchini Qatar
Neymar Jr
Mbrazili huyu ambaye anaichezea PSG ya huko Ufaransa alitangaza kushiriki kombe la dunia nchini Qatar kwa mara ya mwisho licha ya kuwa na miaka 30 pekee. Utofauti wake Neymar juu ya kustaafu soka ni kutokana na msukumo na hisia anazokuwa nazo juu ya mashindano hayo na kuona kwa yeye inatosha kabisa baada ya Qatar.
Wanasoka wengi katika awamu hii wataachana na soka kutokana na umri wao kusonga mbele na hili linaweza kuwapigo kubwa kwa mashabiki wao ambao bado wana matumaini na wachezaji hao ila moyo ndo umeshataka na mwili umechoka hivyo kila laheri kwao.
Leave your comment