Nyimbo Mpya: Billnass 'Puuh',Harmonize 'Mwenyewe' na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Wasanii kutoka nchini Tanzania wameendelea kukoleza burudani kwa mashabiki zao kwa kuachia ngoma kali ambazo zina lengo la kuchangamsha na kufanya mashabiki wafurahi.

Katika kiwanda cha muziki ambacho kila siku kuna ngoma mpya inatoka, tumekuandalia ngoma ngoma 5 mpya ambazo zimetoka nchini humo kwa wiki hii kutoka kwa wasanii tofauti tofauti ikiwemo Billnass, Tommy Flavour na wengineo wengi.

Puuh - Billnass Ft Jay Melody

Kwenye ngoma hii ya "Puuh" utapenda kila kitu kuanzia beat mpaka mashahiri lakini hasa utavutiwa na kiitikio kizuri kutoka kwa Jay Melody ambaye kwa mujibu wa Billnass, Jay Melody alirekodi kiitikio cha wimbo huo ndani ya dakika 3 tu.

Tangu kuachiwa kwake Puuh imepokelewa vizuri sana na mashabiki hasa kutokana na Puuh Challenge ambayo imejizolea umaarufu mkubwa sana mtandaoni

https://www.youtube.com/watch?v=3qN9A3XIPcw

The Kid You Know (Album)  - Marioo

Baada ya kusubirisha mashabiki kwa muda mrefu hatimaye wiki hii Marioo aliachia albamu yake ya "The Kid You Know" ambayo ndani yake Marioo amefanya Amapiano, R&B, Afro Beats, Kizomba pamoja na Bongo Fleva huku akiwa amewashirikisha wasanii kama Ali Kiba, Rayvanny, Jovial na wengineo wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=doA6FP-Mvgc

Whine For Me - Tommy Flavour Featuring Vanillah Music

Tommy Flavour hakuwa anatania aliposema kwamba kwa sasa yeye ndiye mfalme wa R&B na wimbo wake huu mpya wa kuitwa "Whine 4 Me" akiwa na msanii mpya wa Kings Music wa, Vanillah, umethibitisha hilo. Kwenye ngoma hii utapenda kila kitu kuanzia  mashahiri mpaka mdundo wake uliojaa uraibu wa aina yake.

https://www.youtube.com/watch?v=aYWqBc98xXs

Mwenyewe (Video) - Harmonize

Kutoka kwenye albamu yake ya Made For Us, Harmonize hatimaye ameachia video ya "Mwenyewe" ambayo inafanya vizuri sana. Kilichokosha wengi kuhusu ngoma na video hii ya "Mwenyewe" ni uhalisia wake kwani Harmonize kwenye ngoma hii anazungumzia kuhusu maisha halisi.

https://www.youtube.com/watch?v=6xljT0q1-Lc

 

Ohooo - Mimi Mars Featuring Baddest 47

Kutoka kwenye himaya ya Mdee Music Mimi Mars ameachia ngoma yake kali ya kuitwa Ohoo akiwa amemshirikisha Baddest 47. Hii ni ngoma ya kwanza ya Mimi Mars ndani ya miezi 6

https://www.youtube.com/watch?v=MMj76YDb_ao

Leave your comment

Top stories