Mavokali Athibitisha Ngoma Yake Kutumika Na Dj Khaled Wa Marekani

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutokea nchini Tanzania Mavokali hivi karibuni amethibitisha kwamba Dj maarufu kutokea nchini Marekani, DJ Khaled, alitumia wimbo wa Commando ambao kwa sasa unatamba pande zote za Tanzania.

Wimbo wa Commando wa kwake Mavokali ulitoka mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka 2022 na tangu kuachiwa kwake, Commando imeweza kupenya nchi mbalimbali duniani kupitia Shazam ambapo iliweza kusikilizwa kwenye nchi kama Romania, Costa Rica, Saudi Arabia, Peru na nchi nyingine nyingine.

Akizungumza hivi karibuni na Lil Ommy kwenye Refresh, Mavokali alithibitisha kwamba ni kweli Dj Khaled alionekana akiwa anacheza na kufurahia ngoma yake ya Commando na kwamba, video ile iliyokuwa ikisambaa mtandaoni ni ya kweli na sio ya kutengenezwa.

"Ile ni video ya ukweli bro. Mpaka akaunti inakuwa verified huwezi kuposti kitu cha uongo. Cha kwanza hicho. So amepost ile clip ametumia sauti yangu kwenye akaunti yangu na ukiangalia ile ngoma alikuwa ana vibe ngoma yangu kwa sababu kuna sauti ukisikiliza vizuri zinasikika kwa chini" alizungumza Mavokali.

Leave your comment