Diamond Platnumz Atangaza Kuachia 'Yataniua' Remix

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz kwa mara nyingine ametikisa kiwanda cha Bongo Fleva baada ya kutangaza kwamba Mbosso anatarajia kuachia remix ya ngoma yake ya "Yataniua"

Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni alishinda tuzo ya AFRIMMA kama mtumbuizaji bora Afrika ametangaza kuhusu ujio wa Yataniua Remix hivi karibuni ikiwa ni wiki takriban mwezi mmoja tangu Mbosso aachie EP yake ya "Khan". Yataniua ni ngoma namba 6 kwenye EP ya Mbosso ya kuitwa Khan na ni moja kati ya ngoma pendwa baina ya mashabiki.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diamond Platnumz alitangaza kwamba Yataniua Remix inatarajiwa kuingia sokoni Ijumaa hii na kisha kudokeza kuhusu msanii ambaye atashirikiwa kwenye remix hiyo ambayo inasubiriwa mno na mashabiki.

" Yataniua …… Yes We Dropping Yataniua Remix this Friday. Guess who is featured?" aliandika Diamond.

Ikumbukwe kuwa ngoma ya Yataniua ilishushwa kwenye mtandao Youtube kutokana madai ya hatimiliki ambapo wengi waliufananisha wimbo huo na wimbo wa "Peace Be Unto You" pamoja na "Adiwele" ya Young Stunna.

Kando na ngoma hii ya Yataniua, Diamond Platnumz kwa mwaka 2022 ameshirikishwa kwenye ngoma kama "Hadithi" ya Barnaba Classic, "Nitongoze" ya Rayvanny pamoja na Kolo Kolo ya Patoranking, msanii kutokea huko nchini Nigeria.

https://www.youtube.com/watch?v=KhNzgS38c3Y&list=PLVTehZ7qhaEPreHrakLu4Mq2YPaSwQF2D

Leave your comment