Southgate Athibitisha Uwepo wa Harry Kane Mechi Dhidi ya USA - Mdundo Alt

[Picha:Sports Mole]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Katika mchezo wa awali wa kundi B ulioikutanisha Uingereza pamoja na Iran katika uwanja wa Al Janoub ambao ulimalizika kwa ushindi wa mabao 6-2 kutoka kwa Uingereza ulimfanya straika wa timu hiyo Harry Kane kutolewa nje ya mchezo kutokana na majeraha ya goti la kulia.

Siku ya Jumatano taarifa za kuhuzunisha zikajiri katika timu hiyo ya Taifa ya Uingereza ya kuwa mchezaji huyo kutokea Tottenham Hotspurs atalazimika kupitia vipimo ili kujua ukubwa wa tatizo lake hilo la goti kabla ya kuendelea na mchezo mwingine na timu yake ya Taifa.

Siku iliyofuata kocha wa kikosi hicho Gareth Southgate akathibitisha ya kuwa Harry Kane ambaye pia ni nahodha wa kikosi hicho kushiriki mechi inayofuata ambayo itawakutanisha dhidi ya USA ambao wao katika mchezo wao wa awali walitoka sare ya bao moja kwa moja katika mchezo waliocheza na Wale.

Katika kundi B ambalo linahusisha timu nne, Uingereza wanaongoza kundi hilo wakifuatiwa na USA pamoja na Wale ambao wao wana alama moja kwa kila timu na Iran wakishika nafasi ya mwisho baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Uingereza.

Leave your comment