WorldCup: Ripoti mechi ya Brazil Vs Serbia - Mdundo Alt
25 November 2022
[Picha:Sporting News]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Washindi mara tano wa kombe la dunia Brazili, wameanza vizuri mashindano hayo baada ya kushinda katika mechi yao ya kwanza katika kundi G mara baada ya kuwatandika Serbia mabao 2-0 mechi iliyochezwa katika uwanja wa Lusail.
Miamba hao ambao wanajulikana pia kama Selecao walifanikiwa kupata mabao yote mawili kupitia kwa Richarlson ambaye pia anachezea timu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza baada ya kipindi cha pili cha mchezo kuanza. Bao la kwanza lilifungwa katika dakika ya 62 na bao la pili likazua gumzo zaidi baada ya Richarlson kupokea pasi kutoka kwa Vinicius Jr na kupiga Tiktaka makini sana na kuwaka bao hilo kambani.
Baada ya mchezo kukamilika Richarlson ndiye akaibuka mchezaji bora katika mchezo huo ambapo pia kuchaguliwa kwake kujiunga na kikosi cha Brazil ni baada ya kupona majeraha aliyoyapata wakati akiwa na Spurs na hii ikathibitisha kuwepo kwa kiwango chake uwanjani.
Brazil wakiongozwa na nahodha wao anayetokea Chelsea Thiago Silva walicheza mchezo huo kwa nidhamu ya hali ya juu na kumaliza mechi hiyo bila kadi yoyote ukilinganisha na Serbia walioondoka na jumla ya kadi tatu za njano.
Wanasamba hao kutokea Rio de Janeiro walifanikiwa kuutawala mpira kwa asilimia 63 na kuwaachia 36% vijana wa Dragan Stojkovic katika umiliki wa mpira.
Kwa sasa kundi G linaongozwa na Brazil wakiwa na alama tatu wakifuatiwa na Uswizi wenye alama tatu pia baada ya kuwafunga Cameroon wenye alama sifuri na Serbia wao wakiburuza mkia wakiwa pia na alama sifuri.
Leave your comment