Nyimbo Mpya: Marioo Aweka Wazi Historia Ya Maisha Yake Kwenye Ngoma Mpya "My Life"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama ulikuwa na hamu na shauku ya  kumsikia Marioo basi ondoa shaka kwani tayari msanii huyo kutoka kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva ameshaachia mkwaju wake mpya wa kuitwa "My Life"

Kwa mujibu wa Marioo ambaye mapema mwaka huu alishinda tuzo ya msanii bora wa Bongo Fleva kwenye tuzo za Tanzania Music Awards, msanii huyo amedokeza kwamba "My Life" ndio ngoma ya kwanza kutoka kwenye album yake ya The Kid You Know ambayo inatarajiwa katika mitaa siku zijazo.

My Life ni ngoma ambayo Marioo anadokeza kuhusu maisha yake. Namna ambavyo alianza muziki, changamoto alizopitia ikiwemo watu waliomkatisha tamaa huku mwanzoni kabisa ya wimbo huu, Marioo anaoneaha hisia mseto alizonazo kwa kusema kwamba  "Nabii Hakubaliki Kwao" msemo ambao unaakisi jinsi ambavyo baadhi ya mashabiki hukosa kuwapa thamani wasanii wa nyumbani.

My Life ni ngoma ya 5 kwa Marioo kwa mwaka huu baada ya Naogopa akiwa na Harmonize, Yanga Anthem pamoja na Amapiano zake mbili zilizoteka taifa yaani Dear Ex pamoja na Sina Baya.

https://www.youtube.com/watch?v=B1lGCNy2xBY

Leave your comment