Rayvanny Aachia Ep Mpya Inayoitwa "Unplugged Session"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutoka Tanzania na CEO wa, lebo ya Next Level Music, Rayvanny kwa mara nyingine ameweka historia baada ya hivi karibuni kuachia EP ambayo ameipa jina la "Unplugged Session".

Rayvanny ambaye siku kadhaa nyuma aliweka historia baada ya kushinda kipengele Msanii bora wa kiume Afrika Mashariki ameachia EP hiyo ya Unplugged Session bila kufanya promotion yote mtandaoni au kwenye vyombo vya habari, kitu ambacho pia alishawahi kufanya mwaka 2021 wakati alipoachia EP yake ya New Chui.

Unplugged Session ni kazi ambayo imesheheni ngoma 8 na kati ya hizo ni ngoma moja tu ambayo Rayvanny amemshirikisha msanii mwingine ikiwa ni ngoma namba 8 ya kuitwa Nipigie ambayo amemshirikisha Dar Kid. Ngoma nyingine zilizopo kwenye Unplugged Session ni pamoja na Mzuri, I Love You, Nateswa na nyinginezo nyingi.

Aidha ngoma hizo pia zimesindikizwa na video kali ambapo kati ya ngoma hizo 8 tayari Rayvanny ameshaachia video ya ngoma zote ambazo kwa sasa zinapatikana kwenye mtandao wa Youtube. Unplugged Session ni mradi wa pili wa Rayvanny kuachia baada ya kutoka WCB kwani siku chache nyuma aliachia ngoma yake ya Nitongoze ambayo alimshirikisha Diamond Platnumz.

https://www.youtube.com/watch?v=VKgRB1eU8Mc

Leave your comment