Diamond Platnumz Afichua Siri Ya Wasanii Kutoka Nigeria Kufanya Show Kubwa Nchini Marekani

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Nyota wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz kwa mara nyingine ameingia kwenye vichwa vya habari Tanzania baada ya kuweka wazi sababu zinazopelekea wasanii kutokea nchini Nigeria kufanya matamasha makubwa Marekani na nchi nyingine za ughaibuni.

Kwa miaka ya hivi karibuni wasanii kutokea nchini Nigeria kama Wizkid, Davido pamoja na Burna Boy wamekuwa wakifanya matamasha makubwa ya muziki kwenye kumbi kubwa duniani kama O2 Arena pamoja na Madison Square Garden, kitu ambacho kufikia sasa hakuna msanii yoyote kutokea Tanzania ameshawahi kufanya.

Akizungumza hivi karibuni kwenye Masterclass iliyoandaliwa na Ziiki Media Diamond Platnumz amefichua kwamba moja ya sababu inayochagiza wasanii kutoka Nigeria kufanya matamasha makubwa Marekani na nchi nyingine ni kutokana na uwepo wa Diaspora wengi kutoka Nigeria  katika nchi hizo.

"Sasa hivi mtu a nakwambia inabidi uende Madison ukajaze, we pale baba yako yupo atakuja kwenye show? Wale wenzetu wa Magharibi watu wengi wanaokuja kwenye show zao ni wao wenyewe kwanza. Wako wengi sisi wametuzidi. Kwa hiyo tuna tatizo la kwamba wao wako wengi nje sisi tuko wachache." alizungumza Diamond Platnumz.

Aidha Diamond Platnumz pia alidokeza, kwamba baadhi ya mashabiki wa muziki Tanzania waache kuwalaumu wasanii wa nyumbani badala yake wawashike mkono kwa kusikiliza ngoma zao kwenye majukwaa mbalimbali ya kusikilizia muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=mgvI82Uhql8

Leave your comment