Moni Centrozone Aachia 'Toto' Akiwa Na Country Wizzy

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Moni Centrozone kwa mara nyingine amezidi kuonyesha uwezo alionao kwenye muziki wa hip hop baada ya kuachia ngoma yake mpya inayoitwa 'Toto' ambayo amemshirikisha Country Wizzy.

Ikumbukwe kuwa Moni Centrozone ambaye kwa sasa anasimamiwa na Rooftop Entertainment alikuwa hajaachia ngoma yoyote kwa takribani miezi miwili tangu aachie ngoma ya 'Read Again' ambayo alimshirikisha rapa na mwanamuziki kutokea kundi la Weusi, G Nako.

'Read Again' ni ngoma nyingine ambayo Moni Centrozone haoni hatari kututembeza, na kuturudisha kwenye mtindo wake wa kawaida wa kurap ambao upo katikati ya Bongo Hip Hop au Hip Hop Mambo Leo yaani Trap. Midondoko pamoja na mipangilio ya sauti bila shaka inatukumbusha ngoma zake za zamani ikiwemo Cha Mbunge.

Mashahiri ya ngoma ya Toto yanamsifia binti mrembo ambaye kuanzia mitindo yake ya kuvaa mpaka namna ambavyo anajiweka, Moni anakiri kwamba hivyo ni vitu ambavyo vinampagawisha sana.

Ngoma hii ambayo inatarajiwa kuteka Tanzania imetayarishwa na S2kizzy, mtayarishaji wa muziki ambaye kufikia sasa ameshafanya kazi na wasanii tofauti tofauti Tanzania ikiwemo Zuchu, Diamond Platnumz, Rayvanny na wengineo wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=8ZhhS5Ywk2I

Leave your comment