Hatimaye Glazer Wanyoosha Mikono Juu Kuiuza United - Mdundo Alt

[Picha:Sky Sports]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Hatimaye pumzi itaanza kuwashuka mashabiki wa timu ya Manchester United baada ya timu hiyo kudokeza kuwa familia ya Glazer kutaka kuiuza  klabu hiyo ambayo wamekuwa wakiimiliki Kwa miaka 17 iliyopita.

Kwa ukubwa wa klabu hiyo inasemekana dau la Euro bilioni tano limetangazwa Kwa mnunuzi atakayekuwa na nia ya kununua timu hiyo. Mwaka 2005 Glazer waliinunua United Kwa jumla ya Euro million 780.Dau Hilo pia litahusisha maboresho katika klabu hiyo hususa ni katika maboresho ya uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford.

Mashabiki wa timu hiyo kwa muda Sasa wamekuwa wakipinga wamiliki wa klabu hiyo wakiwatuhumu kutumia fedha za klabu kulipa riba za madeni yao na kushindwa kufanya mipango endelevu ya maboresho ya Klabu hiyo.

huu unaweza kuwa wakati mahususi Kwa mashabiki hao kurejesha walau furaha yao baada ya taarifa hiyo. Mwaka 2021 mechi ya Liverpool waliotarajiwa kucheza dhidi ya mashetani hao wekundu ililazimika kughairishwa baada ya mashabiki kuleta vurugu.

Katika maelezo ya klabu Hilo waliyoyatoa kupitia tovuti Yao waliandika ya kuwa '....bodi itazingatia mikakati mbadala ikiwemo uwekezaji mpya katika klabu, mauzo au miamala mingine itakayohusisha kampuni....'

Taarifa hii pia imeambatana na Ile ya Cristiano Ronaldo ya kukubaliana na klabu hiyo kuondoka klabuni hapo baada ya mahojiano yake na Piers Morgan ambayo pia aliitaja familia ya Glazer kutokujali timu hiyo na kuweka maslahi yao binafsi.

Leave your comment