Ripoti Mechi Ya Ufaransa Vs Australia- Kundi D

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mabingwa watetezi wa kombe la dunia Ufaransa wameanza vizuri mashindano hayo mara baada ya kuondoka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Australia mechi iliyochezwa katika uwanja wa AL Janoub.

Australia walianza mchezo huo kwa kasi ya hali ya juu mara baada ya wao kutangulia kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Craig Goodwin baada ya dakika nane pekee za mchezo na hali hii ikaiamsha Ufaransa na kuzidisha mashambulizi kwa Australia.

Kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika kiungo kutokea Juventus Adrien Rabiot alisimamisha tumaini la Ufaransa baada ya kusawazisha katika dakika ya 27 ya mchezo na magoli mengine kufungwa na Kylian Mbappe katika dakika ya 67 baada ya kufanikiwa kuipata krosi kutoka kwa Dembele na hili kuwa ndio bao la kwanza katika mashindano haya ya kombe la dunia.

Mchezaji bora wa mechi hiyo alikuwa ni straika Olivier Giroud ambaye ni kipenzi cha wafaransa wengi mara baada ya kufunga mabao mawili katika dakika ya 31 pamoja na ile ya 72 . Staika huyo ambaye pia alikuwa na Ufaransa wakati wa ushindi wa kombe la dunia mwaka 2018 amejiwekea rekodi yake mara baada ya kuwa na jumla ya mabao 51 katika mechi zote alizoshiriki na timu hiyo ya Taifa

Licha ya kutangulia kufunga Australia walipata umiliki mdogo wa mpira dhidi kwa Ufaransa baada ya kuwa na 38% wakizidiwa na Ufaransa waliokuwa na 62%. Kwa hali hii waliyoanza nayo Ufaransa inaweza kuwa nyota njema ya kutaka kuutetea ubingwa wao huo wa dunia kwa mara ya pili mfululizo. Katika kundi D ufaransa wanaongoza walifuatiwa na Denmark pamoja na Tunisia waliotoka sare ya bila kufungana huku Australia wakiburuza mkia.

 

Leave your comment