Manchester United Wakubaliana Kuvunja Mkataba na Cristiano Ronaldo- Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya kufanya mahojiano yake na Piers Morgan na kueleza hisia zake juu ya Manchester United na changamoto alizozipitia, sasa timu hiyo  imetoa tamko juu ya moja kati ya washambuliaji wakali zaidi kwa muongo uliopita Cristiano Ronaldo na kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba.

Hili linaweza lisiwe jambo geni sana mara baada ya mchezaji huyo kutaka kuondoka katika klabu hiyo mashuhuri dunia wakati wa dirisha kubwa la usajili na timu hiyo kugoma na kusema ya kuwa bado ina mipango dhidi yake ikiwa chini ya kocha Erik Ten Hag.

Katika maelezo hayo klabu ya Manchester United iliandika ya kuwa …..Cristiano Ronaldo ameondoka kwa makubaliano ya pande zote mbili na pia klabu inamshukuru kwa mchango wake wa vipindi vyote viwili………’. Ikubukwe pia Ronaldo alijiunga na United mwaka 2003 akitokea Sporting Lisbon ya Ureno kabla ya kujiunga na Real Madrid ya Uhispania mwaka 2009.

Baada ya mahojiano hayo moja kati ya mambo yaliyoleta mzozo na kuzua mgawanyiko ni pamoja ya utofauti uliokuwepo kati kocha wa United pamoja na mshindi huyo wa tuzo za Ballon d’or baada ya Ronaldo kusema ya kuwa hakuna heshima juu yao.

Baada ya taarifa hiyo pia familia ya Glazier ambao pia ni wamiliki wa klabu hiyo inasemekana huenda wakaiuza Manchester United na pia Cristiano Ronaldo katika mahojiano yake na Piers Morgan aliitaja familia hiyo ya Glazier kutokuijali timu hiyo na wao kuangalia maslahi ya kifedha pekee.

Ni wapi mchezaji huyo nguli wa soka atakimbilia?

Hili ni swali ambalo limebaki bila majibu ya moja kwa moja kwani mpaka sasa hakuna timu iliyotajwa wazi kumtaka mchezaji huyo na huenda Bayern Munich wakaupata mchango wa straika huyo hapo Januari lakini kwa sasa Manchester City sidhani kama ina nafasi tena kwa Ronaldo baada ya kumsajili Erling Haaland. Vilabu vingine vinavyohusishwa na kumsajili Ronaldo ni pamoja na Atletico Madrid, Newcastle United pamoja na AC Milan.

Leave your comment