Saka, Bellingham Wachezaji wa Uingereza Waliongara World Cup - Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mashindano ya kombe la dunia yanaendele huko Qatar ikiwa siku ya Jumatatu Uingereza iliweza kunyakua alama tatu za mapema mara baada ya kumpa kichapo cha bao 6 kwa 2 Iran.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Taifa wa Khalifa ulimfanya Iran azidiwe mbinu na Uingereza kwa asilimia 76 ya mchezo huku Iran wakimiliki mpira kwa asilimia 24 pekee.

Katika mchezo huo nyota kutokea Arsenal, Bukayo Saka aliondoka katika mchezo huo kama nyota baada ya kuonesha uwezo wake na kuwa sehemu ya mabao mawili ya mchezo kati ya yale sita na magoli mengine kufungwa na Marcus Rashford, Raheem Sterling, Jack Grealish, na bao la ufunguzi likifungwa na kinda kutokea Borussia Dortmund Jude Bellingham. Hili  ni bao la kwanza kwa Bellingham akiwa na Uingereza kwa mara ya Kwanza.

Mabao mawili ya Iran yalipatikana katika kipindi cha pili kutoka kwa Mehdi Taremi katika dakika ya 65 na kuwaamsha Uingereza waliokuwa wameanza kupoa.

 Katika dakika za nyongeza bao la pili likafungwa kwa Penalti baada ya John Stone kumfanyia madhambi Mehdi Taremi ndani ya eneo la hatari na mchezaji huyo akaweza kujipatia bao lake la pili katika mchezo huo.

Huu ni mwanzo mzuri kwa Gareth Southgate wakiwa sasa wanaongoza kundi B kabla ya kukutana na Wale ambao walitoa sare dhidi ya USA katika mchezo uliochezwa siku ya Jumatatu.

Mwaka 2021 Bukayo Saka pamoja na Marcus Rashford ni kati ya wachezaji waliopitia ubaguzi wa rangi katika fainali za mashindano ya Euro 2020 baada ya kukosa penalti na kupoteza mbele ya Italy, huu unaweza kuwa mwanzo mzuri kwa mashabiki wao ambao waliwarushia maneno yasiyofaa mitandao.

Leave your comment