Christina Shusho Aachia Tracklist Ya Albamu Yake Ya "Hararat"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Baada ya subira ya muda mrefu hatimaye mwanamuziki kutokea Tanzania, Christina Shusho ameachia tracklist rasmi ya albamu yake ya kuitwa Hararat ambayo alitangaza kuiachia hivi karibuni.

Christina Shusho ambaye ana miaka zaidi ya kumi kwenye tasnia ya muziki nchini ameachia orodha hiyo ya nyimbo pamoja na wasanii walioshirikishwa kwenye albamu yake hiyo ya Hararat, takriban wiki mbili tangu atangaze kwamba yuko mbioni kuachia albamu yake mpya kabisa.

Albamu ya Hararat imesheheni ngoma 25 ambazo ndani yake, Christina Shusho ambaye alitajwa kuwania tuzo za AFRIMMA mwaka 2022 ameshirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo Benjamin Weston, Anitha Musoki, Mercy Masika kutokea Kenya, Sammie Okposo kutokea Nigeria, Alarm Ministries kutokea Rwanda na wasanii wengine wa ndani na nje ya Tanzania.

Kwa mujibu wa Christina Shusho kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni, alidokeza kuwa albamu yake inatarajiwa kuachiwa mwanzoni mwa mwaka wa 2023 hivyo mashabiki wakae tayari kupokea ujio wake mpya.

Leave your comment