Vifahamu Viwanja 8 Mahususi Kwa Ajili Ya Kombe la dunia - Qatar -Mdundo Alt

[Picha:Aljazeera]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Subira yavuta heri, ni katika kombe la dunia ambalo litaanza kwa timu za Taifa kupaperusha bendera za nchi zao Jumapili ya wiki hii. Qatar inasemekana imetumia zaidi ya dola milioni 200 katika kuanza mashindano hayo ambapo fedha hizo zimetumika katika kuboresha na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo viwanja vya mpira Vifuatavyo ni viwanja nane ambavyo vitatumika katika mashindano hayo ya kombe la dunia.

 

Uwanja Wa Kimataifa Wa Khalifa

Mnamo mwaka 2017 ndipo uwanja huu ulianzishwa ukiwa unapatikana katika mji mkuu wa Doha na kupewa jina la Khalifa kama moja ya kumuenzi Amir khalifa bin Hamad al Thani. Uwanja huu unauwezo wa kumudu jumla ya watu 40000. Pia timu ya Taifa ya Qatar huutumia uwanja huo kama uwanja wao wa nyumbani. Katika uwanja huo mechi zitakazochezwa ni mpaka zile za mshindi wa tatu na nne wa kombe la dunia.

 

Uwanja Wa Al Janoub

Ulianzishwa mwaka 2019 katika mji wa Al Wakrah ambalo pia ni jina la mwanzo la uwanja huo. Unauwezo wa kuingiza jumla ya watu 40000 kwa pamoja. Uwanja huo wa Al Janoub utatumika katika mechi za 16 bora katika kombe la dunia.

 

Uwanja Wa Ahmad Bin Ali (Al Rayyan)

Ni uwanja unaotumika katika michezo mbalimbali uliopo mji wa Al Rayyan, Qatar. Uwanja huu ulianzishwa Mei 2020 na unauwezo wa kumudu jumla ya watu 40000. Katika kombe la dunia uwanja huu utatumika mpaka katika mechi za 16 bora.

 

Uwanja Wa Education City

Unapatikana katika mji wa Al Rayyan ukiwa umezungukwa na baadhi ya vyuo vya mji wa Al Riyyan. Uwanja huu ulijengwa mwaka 2020 kama moja ya viwanja vitakavyotumika Katika mashindano ya kombe la dunia nchini Qatar. Uwanja wa Education City utatumika mpaka Katika mechi za robo fainali ukiwa na uwezo wa kuingiza watazamaji 40000.

Uwanja Wa 974

Ni uwanja wa muda uliojengwa mwaka 2021 na jumla ya makontena 974  ukiwa ni uwanja wa kwanza kutengezwa kwa muda katika mashindano ya kombe la dunia. Uwanja huu uko katika jiji la Doha ambapo utatumika katika mechi saba za kombe la dunia mpaka mechi za timu 16 bora. Jumla ya watu 40000 wanauwezo wa kuingia katika uwanja huu.

Uwanja Wa Al Thumama

Ni moja kati ya viwanja vilivyojengwa mahususi kwa ajili ya kombe la dunia. Uwanja huu ambao uko karibu na kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Hamad kinauwezo wa kuwa na washangiliaji 40000 ambacho kitatumika mpaka mechi cha robo fainali.

Uwanja Wa Al Bayt

Katika jiji la Al Khor ndipo uwanja huu unapopatikana ambao unauwezo wa kuingiza watu 60000. Uwanja huu ulianzishwa Mei 2021 na katika kombe la dunia uwanja huu utatumika katika mechi za ufunguzi pamoja na zile za nusu fainali katika kombe la dunia.

Uwanja Wa Lusail

Huu ndio uwanja mkubwa kuliko yote nchi Qatar ambao pia utatumika katika fainal za kombe la dunia. Jumla ya watu 80000 wanauwezo wa kuingia katika uwanja wa Lusail na kushuhudia kombe la dunia. Ujenzi wa uwanja huu umekamilika mwaka 2022. Baada ya kombe la dunia uwanja wa Lusail utatumika katika shughuli za kijamii kama  vile ujenzi wa shule, vituo vya afya, vituo vya michezo, pamoja na maduka.

Leave your comment