Qatar Kutokukidhi Vigezo Vya FIFA 2010 - Mdundo Alt
11 November 2022
[Picha: skysports]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Rais wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA, Sepp Blatter ambaye aliongoza shirikisho hilo kuanzia mwaka 1998 mpaka 2015 na kusimamishwa kutokana na tuhuma za rushwa mapema wiki hii amekiri kuipatia Qatar nafasi ya kuwa wenyeji wa kombe la dunia kinyume na sheria.
Mnamo mwaka 2010 Qatar ndio waliteuliwa kuwa wenyeji wa kombe la dunia lakini wiki hii Blatter katika jarida moja la habari nchini Uswizi alisema ya kuwa baada ya Urusi, USA ndiyo iliyotakiwa ifuate kuwa wenyeji wa kombe hilo la dunia litakalofanyika mwezi Novemba mwaka huu na kusema pia ni makosa aliyoyafanya katika chaguo hilo la Qatar.
Katika mahojiano na gazeti la Tages-Anzeiger Blatter aliongeza kwa kusema ‘... Qatar kupata nafasi ya kuwa wenyeji ni makosa na mimi nilikuwa na jukumu kama Rais wa wakati huo.’ Pia Rais huyo wa zamani alisema ya kuwa hana uhusiano na Rais wa Urusi kwa sasa na kuoneshwa kukerwa na uvanizi wa Urusi nchini Ukraini.
Baada ya kombe la dunia la nchini Qatar kukamilika huenda USA wakapata nafasi ya kuwa wenyeji wa kombe la dunia linalofuata litakalo fanyika mwaka 2026 kwa sasa wakiwa kinyang’anyironi na nchi kama vile Mexico, Canada na wenyewe USA.
Mwaka 2015 Sepp Blatter alisimamishwa katika nafasi yake ya Urais wa shirikisho la soka duniani kwa tuhuma za rushwa na kufanya azuiliwe kushiriki shughuli zozote za soka tangu kipindi hicho.
Leave your comment