Christina Shusho Atangaza Kuachia Albamu Mpya

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Injili kutokea nchini Tanzania Christina Shusho hivi karibuni ametangaza kwamba yuko mbioni kuachia albamu yake mpya ambayo kwa muda sasa amekuwa akidokeza ujio wake.

Nyota huyo wa muziki wa Injili ambaye kwa muda sasa amekuwa kimya bila kutoa wimbo wowote ametoa taarifa hiyo wakati akiongea na chombo kimoja cha habari nchini Tanzania ambapo amedokeza kuwa anatarajia kuachia albamu yake mwanzoni mwa mwaka 2023 na kwamba tayari ameshamaliza kurekodi.

"Tukianza mwaka nawahidi sana albamu kali ambayo haijawahi kutokea Tanzania na ambayo haijawahi kutokea Afrika Mashariki na Kati. Nataka nikuhakikishie kwamba nyimbo zote ziko tayari. Sasa ilikuwa tu mpangilio tumalize hili Tuingie hili." alizungumza Christina Shusho.

Kufikia sasa Christina Shusho ameshaachia albamu na EP mbalimbali kama Nipe Macho, Unikumbuke, Relax, Kwa Kanisa La Kristu na nyinginezo nyingi.

Ikumbukwe pia Christina Shusho ametajwa kuwania kipengele cha msanii bora wa Injili Afrika kwenye tuzo za AFRIMMA, kipengele ambacho pia Joel Lwaga ametajwa kuwania.

Leave your comment