Rayvanny Adokeza Ujio Wa Ngoma Mpya

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Nyota wa muziki kutokea Tanzania Rayvanny kwa mara nyingine amefurahisha mashabiki zake baada ya siku leo kudokeza kuwa yuko mbioni kuachia ngoma mpya kabisa hivi.

Taarifa hii njema kutoka kwa Rayvanny inakuja siku chache tangu CEO huyo wa lebo ya Next Level Music kupokea tuzo ya DIAFA yaani Distinctive International Arab Festival katika hafla ya aina yake ambayo ilifanyika katika jiji la Dubai.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, mshindi huyo wa tuzo za BET, alitangaza kwamba baada ya kuachia Pele siku tatu zilizopita kwa sasa anajiandaa kuachia wimbo wake mpya kabisa. Pamoja na taarifa hiyo bado Rayvanny hajatangaza jina wala tarehe ambayo ataachia ngoma hiyo ambayo inasubiriwa mno na mashabiki.

Ndani ya miezi 3 tangu aachie Pelepele, Rayvanny ameshirikishwa kwenye ngoma na wasanii kama Billnass ambaye alimshirikisha kwenye Utaonaje pamoja na rapa kutokea kundi la Weusi, G Nako ambaye alimshirikisha Rayvanny kwenye ngoma ya Tusipangiane.

Leave your comment