Infantino Na Waraka Kwa Washiriki Wa Kombe La Dunia

[Picha: DW]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Wakati kukiwa na mitazamo pamoja na migongano mbalimbali kuhusiana na kombe la dunia Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino ametoa waraka wa maelezo kwa nchi 32 zinazoshiriki kombe la dunia kwa kuzitaka ziendelee kujikita katika kombe la dunia na kuachana na mitazamo hiyo pamoja na mitafaruko ambayo inakinzana.

Maelezo hayo yaliyoandikwa kwa washiriki hao wa kombe la dunia yametolewa ikiwa zimebaki siku chache kwa kombe la dunia kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi Novemba huko nchini Qatar na kikubwa alichokisisitiza ni usawa pamoja na amani kwa washiriki.

Infantino katika maelezo  yake aliandika ya kuwa’ ….tunatambua ya kuwa kuna changamoto pamoja na magumu mengi yanayoendelea katika siasa duniani…  ‘…..tafadhali tusiruhusu kuuingiza mpira katika mitazamo pamoja na vita vya kisiasa vinavyoendelea…’

Katika waraka huo aliuandika kwa timu hizo za Taifa Gianni hakugusia suala la Qatar kupinga mahusiana ya jinsia moja baada ya nchi Ulaya zikiwemo Wales na Uingereza kupinga amri ya kutovaa baji za makapten wa timu zenye maana ya kuwaunga mkono wapenzi wa jinsia moja.

Pia suala lingine ni migogoro ya kisiasa inayoendelea duniani kote kama vile vita ya Urusi dhidi ya Ukraini ni moja ya mambo ambayo Raisi huyo wa FIFA hajayagusia moja kwa moja katika waraka wake huo.

Leave your comment