Ali Kiba Atambulisha Msanii Mpya Kwenye Lebo Yake Kings Music.

[Picha: Youtube]

Mwandishi: Charles Maganga

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Mwanamuziki nguli kutoka nchini Tanzania Ali Kiba kwa mara nyingine ameingia kwenye vichwa vya habari nchini baada ya kutambulisha msanii mpya kabisa kwenye lebo yake ya Kings Music. 

Ali Kiba ambaye kwa sasa anatamba na ngoma zake mbili yaani Asali na Tile amemtambulisha Vanillah kama msanii mpya kwenye lebo yake ya Kings Music ambapo msanii huyo atajiunga na Abdu Kiba pamoja na Tommy Flavour kwenye lebo hiyo. 

Kabla ya kujiunga na Kings Music Vanillah alikuwa ni kiungo maarufu baina ya wasanii wakubwa nchini Tanzania kwani alihusika katika kuandika ngoma nyingi za wasanii wa Tanzania ikiwemo Utu ya kwake Ali Kiba, ngoma ambayo ilijizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania. 

Jina halisi la Vanillah ni Fanuel Phabian Peter na amezaliwa mwaka 1996 ambapo kipaji chake cha muziki kilianza kuonekana akiwa mtoto. Kufikia sasa aneshafanya kazi na wasanii tofauti tofauti ikiwemo Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Nay Wa Mitego na wengineo huku akiwa amehusika kuandika ngoma kama Hainogi, Gimmie Dat, Utu pamoja na Tamba. 

Aidha Vanillah pia ameachia EP yake mpya inaoyitwa Lis"Listen To Me" ambayo amemshirikisha K2ga na ikiwa imesheheni ngoma sita za moto. 

Leave your comment

Top stories

More News