Wasanii Kutoka Tanzania Waliopata Nominations Tuzo Za AEUSA 2022

Mwandishi: Charles Maganga

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kiwanda cha muziki Tanzania kimeendelea kuvuka mipaka na kufika levo za kimataifa na hii ni baada ya baadhi ya wasanii kutoka nchini humo kupata nominations au uteuzi kwenye tuzo za African Entertainment Awards USA maarufu kama AEAUSA 

Katika toleo la mwaka huu tuzo za AEAUSA zinatarajiwa kufanyika mwezi Desemba huko nchini Marekani ambapo wasanii tofauti tofauti kutoka Tanzania wamechaguliwa kuwania tuzo hizo. Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Zuchu, Anjella, Roma Mkatoliki na wengineo wengi. 

Diamond Platnumz ametajwa kuwania kipengele cha msanii bora wa Afrika, Albamu bora ya mwaka pamoja na msanii bora wa kiume Afrika huku Harmonize amepata kipengele cha msanii bora wa kiume kutokea Afrika Mashariki. 

Zuchu, Maua Sama na Nandy watachuana lwenye kipengele cha msanii bora kike wa Afrika Mashariki huku Anjella kutoka Konde Gang akiwa anawania kipengele cha,msanii bora chipukizi ambapo atapata ushindani mkali kutoka kwa Black Sheriff pamoja na Asake. 

Tasnia ya Hip Hop itawakilishwa na Roma Mkatoliki ambaye yeye anawania kipengele cha msanii bora wa Hip Hop Afrika akichuana na Nasty C, Khaligraph Jones na Sho Madjozi. 

Watanzania wengine wanaowania tuzo za AEAUSA ni ni pamoja na Angel Nyigu, Lizer Classic pamoja na Millard Ayo kutoka Ayo Media. 

Leave your comment

Top stories

More News