Ubelgiji na Sakata Jipya la Majeruhi Kombe la Dunia

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Nyota wa soka anayekichapa kuko Serie A akiwa na Inter Milan, Romelu Lukaku amethibitishwa kupata majeraha katika wakati huu ambao Kombe wa dunia likibakiza siku chache kuanza kutimua vumbi huko Qatar kuanzia mwezi Novemba mpaka Disemba mwaka huu.

Mchezaji huyo mwenye miaka ishirini na tisa amerejea tena katika majeraha mara baada ya kukaa nje miezi miwili na sasa baada ya michezo miwili pekee ya Inter waliyocheza dhidi ya Viktoria Plzen katika hatua za makundi Ligi ya mabingwa Ulaya pamoja na mchezo wao dhidi ya Sampdoria Lukaku anarejea tena benchi na bado taarifa za muda wake wa kutibu jeraha hilo haujatambulika mpaka sasa.

Kwa sasa Lukaku katika timu ya Taifa ya Ufaransa ndio moja ya machaguo ya kwanza katika safu ya mashambulizi ambayo inauwezekano mkubwa sana wa kumkosa katika kombe la dunia, pia huenda majeraha hayo ya paja ya mchezaji huyo yakaleta pengo kubwa kwa mwalimu wa timu hiyo ya Taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez.

Katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ubelgiji siyo Lukaku pekee pia majeruhi mwingine ambaye ni mshambuliaji Alexia Saelemaekers ambaye anasumbuliwa na majeraha ya goti na mapema mwezi huu wa Novemba huenda akarejea katika hali yake ya kawaida.

Timu ya Taifa ya Ubelgiji mwaka 2018 katika kombe la dunia walifanikiwa kuishia katika nafasi ya tatu na kuelekea kombe la dunia la mwaka huu timu hiyo ya Taifa watachuana na Canada, Morocco pamoja na Krashia ambapo timu hizi ziko katika kundi F.

Leave your comment