Historia Ya Quick Rocka : Mambo 5 Usiyoyafahamu Kuhusu Rapa Huyo.
1 November 2022
Mwandishi : Charles Maganga
Download FREE Mp3 Music by Quick Rocka on Mdundo.com
Bila shaka Quick Rocka ni moja kati ya wasanii wa Hip Hop hodari sana katika kiwanda cha muziki nchini Tanzania. Jina lake sio tu kwamba limekua kutokana na kipaji chake cha kurap lakini pia ufundi wake kama mtayarishaji wa muziki pamoja na karama yake ya uigizaji, pia vimechagiza umaarufu wake.
Hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano na Salama, kwenye kipindi cha Salama Na ambacho pia huruka kama Podcast, Quick Rocca alifunguka mengi kuhusu maisha yake ambayo wengi walikuwa hawayafahamu. Yafuatayo ni mambo 5 ambayo ulikuwa hufahamu kuhusu Quick Rocka
Download Salama Na Podcast Episodes on Mdundo.com
Kuingia Kwenye muziki
Quick Rocka alianza kupenda muziki tangu akiwa mtoto ambapo kipindi akiwa shule alikuwa ni mpiga ngoma mashuhuri kwenye bendi ya shule lakini pia alikiwa ni mwalimu kwenye kwaya yao ya Sunday School.
Safari ya muziki ilianza rasmi baada ya kujiunga na kundi linaloitwa Rockas. Baada ya kundi hilo kupata umaarufu mkubwa, Quick Rocka alisainiwa na MJ Records ya Master J kama msanii rasmi ya lebo hiyo.
Kuanzisha Studio Yake Ya Switch Records
Wakati akiwa MJ Records baada ya ngoma yake kuchelewa kufanyiwa mixing and mastering ndipo alipopata wazo la kuwa na studio yake mwenyewe ambayo ilifungiwa rasmi mwaka 2012 na kuitwa Switch.
Tangu kuanzishwa kwake, Switch Records imekuwa kama shule ya kupika watayarishaji wa muziki kwani baadhi ya producers waliopita studio hiyo ni pamoja na S2kizzy, Nahreel wa Navy Kenzo pamoja na Luffa.
Chanzo Cha Jina Lake "Quick Rocka"
Kwenye mahojiano hayo, Quick Rocca, alieleza kuwa kipindi akiwa kwenye kundi la the Rockas alikuwa akijulikana kama "Switch".
Lakini kadri muda ulivyokuwa unakwenda kila mshiriki wa kundi hilo aliamua kupachika jina la "Rocka" baada ya jina lake la kisanii. Na hapo ndipo aliamua kubadilisha jina Switch na kujiita "Quick Rocka" kama ambavyo wenzake walifanya.
Kuhusu Kundi La OMG
Kupitia studio yake ya Switch, Quick Rocka alitambulisha kundi la muziki la kuitwa OMG ambalo lilikuwa limesheheni marapa watatu kama kama Conboi, Salmin pamoja na Young Lunya.
Quick Rocka aliamua kusitisha mkataba na kundi hilo la OMG baada ya kukutana na changamoto mbalimbali ikiwemo za kifedha.
Kuingia Kwenye Uigizaji
Kwa sasa Quick Rocka ni moja kati ya, waigizaji hodari sana Tanzania ambaye anaigiza kwenye tamthilia ya Jua Kali. Lamatta Leah ndiye kwa mara ya kwanza aligundua kipaji cha uigizaji cha Quick Rocca na alimpatia nafasi ya kuigiza, kwenye filamu ya Time After Time ya mwaka 2011, kisha filamu ya Wake Up ya 2014.
Mwaka 2015 alianza kuigiza rasmi kwenye tamthilia ya Kapuni na baada ya kuonesha umahiri wa aina yake mwaka 2019 pia alipata nafasi ya kuigiza Jua Kali, ambayo ni moja kati ya tamthilia bora Tanzania kwa sasa.
Leave your comment