Mbosso Aachia Ramsi Khan EP (Official Video)

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Mwanamuziki kunako lebo ya WCB Mbosso Khan hatimaye ameachia rasmi  EP yake ya kuitwa Khan ambayo kwa muda sasa imekuwa inasubiriwa na mashabiki wa muziki kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. 

Khan EP inakuja wiki chache tangu Mbosso atangaze kuwa anatarajia kuachia EP na tangu hapo, Mbosso amekuwa akidokeza kuhusu ujio wa EP hiyo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania. 

Khan EP imesheheni ngoma sita ambazo ni Huyu Hapa, Pole akiwa na Ruby, Shetani ambayo amemshirikisha Costa Titch na Alfa Kat, Wayo ambayo amefanya na Ya Levis, Assalam ambayo amemshirikisha Mohamed Almanji pamoja na Yataniua ambayo amemshirikisha Diamond Platnumz, ngoma ambayo kwa sasa imeteka watumiaji wengi wa mitabdao ya kijamii. 

Kupitia EP hii Mbosso ameweza kutumia mitindo tofauti tofauti ya muziki ikiwemo Afrobeats, Baibuda Bongo Fleva pamoja na muziki wa Amapiano ambao unasikika kwenye ngoma ya Shetani ambayo 
amefanya na Costa Titch. 

Hii ni EP ya kwanza kutoka kwa Mbosso tangu aanze muziki na inakuja takriban mwaka mmoja na miezi 7 tangu Mbosso aachie albamu yake ya Definition Of Love ambayo imeweza kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania. 

Leave your comment