Otile Brown Tile Uchambuzi
29 October 2022
Baada ya kitambo cha takribani miezi minne kusonga mbele tangu kuachia wimbo wake wa Mama, sasa Alikiba ameamuua kuwaburudisha mashabikii wake wa muziki kwa kuachia tena nyimbo mbili kwa pamoja na zote zikiwa na ujumbe wa mahaba. Tile ni moja kati ya nyimbo hizo mbili ambazo King Ali Kiba ameamua kuwabariki mashabiki wake ukiwa ni wimbo wenye huzuni na majuto mengi katika upande wa suala la mapenzi.
Manunguniko yaliyoka katika wimbo huu yanaufanya wimbo huu uwe na hisia za uzuni zaidi kwa kuwa yanaonesha ni jinsi gani mwandishi anavyopata tabu kurudisha penzi lake kwa Tile na kuibuka na taswira ya msichana aliyeachana naye katika mahusiano hapa awalli. Bado malalamiko na majuto yamezidi kuelezewa hata kwa mifano ili tu Tile aingie tena katika mstari kutokana na maumivu ya kukosa penzi hilo la Tile kama pale aliposema “……..niokoe natapatapa ooh Tile…….” .
Huu ni muziki wa kiba wenye maadhi ya Lingala wenye asili yake huko nchini Congo uliochanganyika na ladha ya Bongo Fleva. Hii si mara ya kwanza kwa mshindi huyu wa tuzo mbalimbali kuwa na ladha hiyo ya muziki kwani hata katika miaka minne iliyopita Mvumo wa Radi pia ulibebwa na maadhi hayo ya Lingala. hata miaka miwili iliyopita Kiba anaonesha kunogewa na maadhi haya ya muziki huo wa Lingala na kuachia wimbo wa Dodo.
Kwa kuwa cha kale dhahabu mwambieni Ali ule uchafu alioutupa wengine wameutumi kama mbolea na mavuno yake si ya muda pungufu. Kwa uchungu aliouonesha Kiba katika wimbo jonzi Tile si ya kuisha hivi punde, penzi uchafu limeanza kunukia kama karafuu iliyotayarishwa kwa lengo la manukato. Akae akijua cha kale dhahabu ila tayari dhahabu hiyo inang’ara kama nyota tayari kambi pinzani wakiishikilia kama punzi yao ya mwisho. Ukisema cha nini sie Twalalama tutakipata lini.
Leave your comment