Ommy Dimpoz Atagaza Kuachia Albamu Yake ya Dedication

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Baada ya subira ya muda mrefu hatimaye mwanamuziki kutokea nchini Tanzania, Ommy Dimpoz ametangaza kuachia albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki ya kuitwa Dedication. 

Taarifa hii kutoka kwa Ommy Dimpoz inakuja wiki kadhaa tangu msanii huyo wa Rockstar Africa adokeze kuhusu ujio wa albamu hiyo ambayo ni ya kwanza kwake tangu aanze harakati za muziki takriban miaka 11 iliyopita. 

Dedication ni albamu ambayo imesheheni ngoma 15 ambapo katika albamu hiyo ameshirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo Nandy, Marioo, Blaq Diamond kutokea Afrika Kusini, Fally Ipupa kutokea Congo, DJ Kerozen, Musa Keys, DJ Maphorisa na wengineo wengi. 

Aidha katika albamu hiyo ya Dedication ni ngoma moja tu ambayo kufikia sasa, imeshatoka na kulingana na Ommy Dimpoz ametanabaisha kuwa albamu yake inatarajiwa kutoka Novemba 4 mwaka huu wa 2022. 

Kando na Ommy Dimpoz, wasanii wengine kutoka Tanzania wanaotarajiwa kuachia albamu hivi karibuni ni pamoja na CEOwa  Konde Music Worldwide, Harmonize ambaye ametangaza kuachia Made For Us tarehe 28 Oktoba pamoja na Marioo ambaye albamu yake ya The Kid You Know inatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.

Leave your comment