G Nako Aachia Ngoma Mpya 'Tusipangiane' Akimshirikisha Rayvanny

Download FreeDJ Mixes on Mdundo.com

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania G Nako kwa mara nyingine ameamua kukata kiu ya burudani kwa mashabiki zake baada ya kuachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa Tusipangiane ambayo amemshirikisha Rayvanny kutoka Next Level. 

Ngoma ya Tusipangiane inakuja takriban miezi 7 tangu G Nako aachie mkwaju wake wa Unakaaje mapema mwezi Machi mwaka huu wa 2022, ngoma ambayo ilipokelewa vizuri sana na mashabiki wa muziki Tanzania. Ngoma 

Kwenye Tusipangiane G Nako na Rayvanny wanatumia maneno na mashahiri ya kuudhi kwa lengo la kupinga tabia ya baadhi ya watu kupendelea kufuatilia kwa undani maisha ya watu wengine na kuwapangia cha kufanya. Kutokana na ujumbe "Tusipangiane" inatarajiwa kuwa maarufu sana kwenye mtandao wa Tiktok ambako watu wengi hupenda kujirekodi wakiimba ngoma za wasanii wao. 

Tusipangiane imetayarishwa na S2kizzy, ambaye pia alihusika kuandaa ngoma ya Tetema ya Rayvanny, Iyo ya Diamond Platnumz, Utaonaje ya Billnass na ngoma nyingine kwenye tasnia ya Bongo Fleva. 

Aidha hii ni collabo ya pili ya Rayvanny tangu aondoke WCB Wasafi kwani tayari kufikia sasa  Rayvanny ameshafanya ngoma ya Utaonaje ya kwake Billnass, ambayo pia imefanya vizuri sana. 

Leave your comment