Abdu Kiba Aachia Ngoma Mpya "Washa" Akimshirikisha K2ga

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye mwanamuziki kutokea lebo ya Kings Music, Abdu Kiba ameachia ngoma mpya kabisa ya kuitwa Washa akiwa amemshirikisha fundi wa muziki, K2ga.

Hii ni ngoma ya kwanza kwa Abdu Kiba ndani ya miezi 7 tangu msanii huyo aachie ngoma ya Sokomoko akiwa amemshirikisha Maua Sama, ngoma ambayo imetoka mwezi Machi mwaka huu wa 2022.

Pakua mziki wa kipekee wake Pastor Anthony Musembi ndani Ya Mdundo

Washa ni ngoma ambayo ndani yake Abdu Kiba anaeleza kwa undani namna ambavyo amezama kwenye penzi zito la mwandani wake, ambapo kupitia ngoma hii Abdu Kiba anatoa sifa moto moto kwa mpenzi wake. Ngoma hii imeundwa na vionjo halisi vya Bongo Fleva huku ikiwa imepambwa na utunzi mzuri wa Abdu Kiba pamoja na sauti ya kuvutia na Abdu Kiba.

Washa imetayarishwa na Mocco Genius kutoka Tanzania, mtayarishaji wa muziki ambaye pia ameaandaa kazi za wasanii mbalimbali kutoka Bongo ikiwemo Ali Kiba, Nandy, Zuchu, Mbosso, Diamond Platnumz na wengineo wengi.

Aidha kupitia ukurasa wake wa Instagram, Abdu Kiba pia amedokeza kuwa video ya Washa inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni kupitia mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=JwDv7gRByKo

Leave your comment