Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Ngoma Ya "Sina Baya"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Marioo ameendelea kuipamba tasnia ya Bongo Fleva baada ya kuachia ngoma yake mpya ya kuitwa Sina Baya ambayo imepokelewa vizuri sana na mashabiki.

Sina Baya ni ngoma ya tatu kutoka kwa Marioo kwa mwaka huu wa 2022 baada ya kuachia Dear Ex pamoja na Naogopa ambayo amemshirikisha CEO wa Konde Music Worldwide, Harmonize.

Download and Stream an all Exclusive Playlist of hits by Latinoh

Sina Baya ni ngoma ambayo Marioo anapita kwenye mdundo mwepesi wa Amapiano, mtindo wa muziki ambao pia aliutumia kwenye ngoma zake kama Mama Amina, Bia Tamu pamoja na Dear Ex. Katika wimbo huu Marioo anasisitiza, kuwa yeye hana ugomvi na mtu yeyote ikiwemo wasanii wakubwa kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Harmonize na hata Rayvanny.

Ngoma hii imetayarishwa na Tony Duardo kutokea Afrika Kusini, mtayarishaji wa, muziki ambaye kufikia sasa ameshafanya kazi na wasanii tofauti tofauti Afrika ikiwemo DJ Maphorisa, Major League, Ciza pamoja na Burna Boy kutokea nchini Nigeria.

Ikumbukwe kuwa Marioo yuko mbioni kuachia albamu yake mpya na ambayo inatarajiwa kuwa albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=hxn0XJJ1ouw

Leave your comment