Nyimbo Mpya: Zuchu 'Kwikwi', Rosa Ree 'Emergency' na Ngoma Zingine Mpya Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama kuna kitu ambacho kinastawisha tasnia ya Bongo Fleva basi ni hulka ya wasanii kuachia ngoma mpya kila wiki ili kuweza kuburudisha mashabiki zao.

Zifuatazo ni ngoma mpya  bora kutoka kwa wasanii wa Tanzania wiki hii :

Kwikwi - Zuchu

Baada ya kuachia Love wiki iliyopita, wiki hii msanii kutokea lebo ya WCB, Zuchu ameachia ngoma yake ya kuitwa Kwikwi ambayo tangj kuachiwa kwake imekuwa maarufu sana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Youtube ambapo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1.

https://www.youtube.com/watch?v=Y2rdmKtVss0

Malafyale - Msamiati Ft Young Lunya

Wiki hii rapa Msamiati aliachia ngoma yake ya Malafyale akiwa amemshirikisha nyota kutoka Rockstar Africa, Young Lunya. Kupitia ngoma hii Msamiati ametoa maarifa mengi kuhusu huku Young Lunya akiwa amepamba ngoma hii na mashahiri ya aina yake.

https://www.youtube.com/watch?v=_beGw41t8XM

Enjoyment - Benpol, Mikky Singer & Gnako

Benpol ameachia ngoma ya Enjoyment akiwa ameshirikisha mkali wa Hiphop Gnako Wara na msanii anayekuja kwa kasi Micky Singer. Ngoma hii ni ya kuchezeka na imepokelewa vyema sana na mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=RaeWlKPUXsE

Noma - Msami

Fundi wa dansi, Msami Baby ameachia ngoma yake mpya ya kuitwa "Noma" ambayo ukiweka kando mashairi yake mepesi lakini pia mdundo wake unatarajiwa kurindima kwenye club na kumbi mbalimbali za starehe hapa Tanzania

https://www.youtube.com/watch?v=WiIUOhGujT8

Emergency - Rosa Ree & Gigy Money

Fundi wa Hiphop kutoka Tanzania, wiki hii ameachia ngoma ya Emergency akiwa na Gigy Money. Kufikia sasa emergency imeshatazamwa mara tisini na tisa elfu kwenye mtandao wa YouTube .z

https://www.youtube.com/watch?v=0POAyenue3k

Zagamua - Baddest 47 Ft Mabantu

Hii ni kazo mpya ya msanni wa Tanzania Baddest 47 ambapo amewaleta pamoja Mabantu ambapo wamewasifia akina dada kwa kujua kiga densi. Zagamua kwa sasa inaendelea kupata umaarufu mtandaoni mashabiki wakipendezwa na kazi ya vijana hawa wenye talanta kubwa.

https://www.youtube.com/watch?v=WeelRVEDYD0

Leave your comment