Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Ngoma Mpya 'Kwikwi'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutoka lebo ya WCB Wasafi Zuchu kwa mara nyingine ametetemesha kiwanda cha bongo baada ya kuachia ngoma mpya kabisa ya kuitwa 'Kwikwi' ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na mashabiki.

Ngoma ya Kwikwi inakuja siku chache tangu Zuchu ambaye ni mshindi wa tuzo ya AFRIMMA kama msanii bora chipukizi mwaka 2020 kuachia ngoma yake ya 'Love' ambayo amemshirikisha nyota kutokea nchini Nigeria na mshindi wa tuzo za Headies 2022, Adekunle Gold.

Kwikwi ni ngoma ya Mapenzi ambayo Zuchu anaonesha ni kwa kiasi gani anampenda mpenzi wake huku akimsihi mpenzi wake huyo asimuache kwani anaogopa kuumbuka na kupata aibu mbele za watu. Tofauti kabisa na Love, Kwikwi ni wimbo wa kuchezeka na unatarajiwa kurindima vilivyo kwenye club na kumbi za starehe mbalimbali.

Kwikwi imetayarishwa na S2kizzy kutokea Tanzania ambaye pia ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kutoka Tanzania kama Vanessa Mdee, Rayvanny pamoja na Diamond Platnumz ambapo amehusika kutengeneza ngoma "Far Away", "Baba Lao" na "Kanyaga"

https://www.youtube.com/watch?v=Yp5FPJwXo0M

Leave your comment