Nuh Mziwanda Aachia Tracklist Ya Ep Yake

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka nchini Tanzania Nuh Mziwanda siku ya leo amezua shangwe kwa mashabiki zake baada ya kuachia rasmi tracklist ya EP yake mpya ambayo inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

Tracklist hii mpya ya Nuh Mziwanda inakuja takribani mwezi mmoja tangu msanii huyo aachie Nampa ngoma ambayo ilipokelewa kwa ukubwa wa aina yake na mashabiki wa muziki wake.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Nuh Mziwanda ametangaza kuwa EP yake inaitwa Wonder na imesheheni ngoma 7 ambazo kati yake ameshirikisha wasanii wakubwa kutoka Tanzania ikiwemo Young Lunya kwenye ngoma Dondosha, Billnass na Mayunga kwenye ngoma ya Show Me Some Love.

Aidha Nuh Mziwanda ameshirikisha watayarishaji mbalimbali wa muziki katika EP yake ikiwemo Paul Maker, Gachi B, Viem pamoja na Dupy Beats ambaye ni moja kati ya watayarishaji bora wa muziki kutoka Tanzania. Wonders EP inatarajiwa kuwa ni project ya kwanza kwa Nuh Mziwanda tangu aanze harakati zake za muziki.

Kando na Nuh Mziwanda wasanii wengine kutoka Tanzania ambao kufikia sasa wameshaaachia EP kwa mwaka 2022  ni pamoja na Kusah ambaye ameachia Romantic EP, Diamond Platnumz ambaye mwezi Machi ameachia First Of All pamoja na Tunda Man.

Leave your comment