Diamond Platnumz Adokeza Kuachia Ngoma Na Costa Titch

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz hivi karibuni kwa mara nyingine ameweza kufurahisha mashabiki zake baada ya hivi karibuni kudokeza kuwa anatarajia kuachia ngoma na msanii Costa Titch kutoka Afrika Kusini.

Taarifa hii kutoka kwa Diamond Platnumz inakuja siku chache tangu msanii huyo atangaze kuwa Ijumaa hii anatarajia kuachia ngoma ya kuitwa ‘Jugni’ akiwa na msanii Diljit Dosanjh kutokea huko nchini India.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya msanii bora Afrika Mashariki kwenye tuzo za Headies, ametangaza kuwa Ijumaa hii ya Tarehe 7  Oktoba, ngoma ya Superstar ambayo ameshirikishwa na Costa Titch kutoka Afrika Kusini itaingia rasmi sokoni.

Ikumbukwe kuwa ni takriban miezi 6 tangu Diamond Platnumz aachie ngoma na wimbo huu wa Superstar unatarajiwa kukoleza orodha ya ngoma ambazo Diamond Platnumz ameshirikishwa kwa mwaka huu. Kando na Costa Titch Diamond Platnumz ameshirikishwa na Barnaba Classic kwenye Hadithi na Patoranking kwenye Kolokolo.

Leave your comment