Nyimbo Mpya: Zuchu 'Love', Alikiba 'Asali' Na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama kuna wiki ndani ya mwaka 2022 ambayo wasanii kutoka Tanzania wameweza kunogesha kiwanda cha Bongo Fleva kwa kuachia ngoma kali basi bila shaka ni wiki hii. Kuanzia kwa Zuchu mpaka kwa Ali Kiba bila shaka hii ni wiki ambayo muziki mzuri umeweza kutawala.

Zifuatazo ni ngoma kali kutoka kwa wasanii wa Tanzania wiki hii :

Love - Zuchu

Hatimaye Zuchu ameachia ngoma ya "Love" ambayo amemshirikisha msanii kutokea Nigeria, Adekunle Gold. Love ni ngoma nzuri ya mapenzi ambayo Zuchu anadhihirisha ni kwa kiasi gani anataka mahaba kutoka kwa mwandani wake.

https://www.youtube.com/watch?v=ECRf_qsQ8jY

Suluhu - Lady Jaydee

Wiki hii Lady Jaydee alikata kiu ya muziki ya mashabiki zake kwa kuachia Suluhu, ngoma ambayo ndani yake Lady Jaydee anamsifia Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na kumsihi kuwa azidi kuunganisha taifa la Tanzania kuwa kitu kimoja.

https://www.youtube.com/watch?v=UKHhPFFsYWA

Tile & Asali - Ali Kiba

Baada ta ukimya wa takriban miezi 11 Ali Kiba wiki hii aliachia ngoma mbili ambazo ni Tile na Asali.

Tile ni ngoma ambayo Ali Kiba anaeleza ni kwa namna gani anataka mpenzi wake wa zamani amrudie, ambapo kupitia sauti yake nzuri, Ali Kiba ameweza kufikisha ujumbe huo.

https://www.youtube.com/watch?v=2bwe9cXvTHs

Asali kwa upande mwingine ni ngoma nzuri ya Mapenzi ambayo ndani yake Ali Kiba anahadithia kwa undani jinsi ambavyo mapenzi ni kitu kizuri kiasi cha kufananishwa na asali.

https://www.youtube.com/watch?v=miGzPizbDFw

Msodoki Young Killer (Albamu) - Young Killer Msodoki

Wiki hii Young Killer ameachia albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki ya kuitwa "Msodoki Young Killer" albamu yenye ngoma 15 na ambayo ndani yake Young Killer ameshirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo Mr Blue, Dreygon, Country Wizzy, Nikki Mbishi na Maarifa.

https://www.youtube.com/watch?v=_05PSfgiUUw

Leave Me Alone - Harmonize Ft Abigail Chams

Akiwa na msanii Abigail Chams kutoka Rockstar Africa, Harmonize alipamba wiki hii na Leave Me Alone, mkwaju ambao umepokelewa vizuri sana na mashabiki hasa kutokana na ujumbe mzuri pamoja na muingiliano mzuri wa sauti baina ya Harmonize na Abigail Chams.

https://www.youtube.com/watch?v=xOSRSlCfPfE

Vacation - Ommy Dimpoz

Kama unataka uende likizo ukiwa na mwandani wako, basi wiki hii Ommy Dimpoz ameachia Vacation ngoma ambayo ina lengo la kuwasindikiza wapenzi pindi wanapokuwa likizo. Ndani ya muda mfupi Vacation imekuwa ni ngoma pendwa baina ya mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=fNALMwI7y6o

Marry Me ( Video) - Barnaba Classic Ft Marioo

Kutoka kwenye albamu ya  Love Sounds Different, wiki hii Barnaba Classic ameachia video ya Marry Me akiwa na Marioo. Video ya Marry Me imeongozwa na Hanscana na tangu kuachiwa kwake imepokelewa vyema na mashabiki.

https://www.youtube.com/watch?v=f-JgVgybiBM

Leave your comment

Top stories

More News