Isha Mashauzi Atangaza Kuachia 'Voice Of Lioness' Ep

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutoka nchini Tanzania wa mziki wa Taarab  Isha Mashauzi kwa mara nyingine ameamua kukonga hisia za mashabiki zake baada ya kutangaza kuachia EP yake ya kuitwa "Voice Of Lioness" hivi karibuni.

Isha Mashauzi ambaye miaka 6 iliyopita alitikisa taifa na ngoma yake ya "Nimpe Nani" anatarajia kuachia EP yake ya Voice Of Lioness ikiwa ni takriban miezi 6 tangu aachie wimbo wa kumsifia Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan uitwao ‘Kazi Iendeleee.’

EP ya Isha Mashauzi imesheheni ngoma 8 ambapo ngoma kama Kazi Iendelee pamoja na Ukinipenda aliyofanya na Banana Zorro, na Stamina Shorwebwenzi tayari zimeshatoka huku ngoma nyingine 6 ambazo ni Umefaulu, Kisorora, Zawadi, Yeke Yeke, Mwache Asome pamoja na Si Levo Yako zikiwa ni mpya kabisa.

[Picha: Instagram]

EP ya Voice Of Lioness inatarajiwa kurudisha hadhi ya Taarab kwenye muziki wa Tanzania ambapo kwa hivi karibuni wadau wengi wa muziki wamekuwa wakilalamika kuwa Taarab, muziki ambao una asili ya huko, Visiwani Zanzibar haupewi kipaumbele kama zamani.

Kando na Isha Mashauzi wasanii wengine kutoka Tanzania ambao wanatarajiwa kuachia EP ni pamoja na Mbosso Khan kutoka lebo ya WCB Wasafi ambaye hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano na Lil Ommy wa Big Sunday Live alithibitisha kuwa anatarajiwa kuachia EP yake muda mrefu.

Leave your comment