Nyimbo Mpya: Alikiba Aachia Ngoma Mbili "Tile" Pamoja na 'Asali'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mfalme wa muziki kutoka Tanzania Ali Kiba kwa mara nyingine ametetemesha kiwanda cha muziki nchini Tanzania baada ya kuachia ngoma mbili kwa mpigo ambazo ni "Tile" pamoja, na "Asali".

Ngoma hizi mbili ambazo zimepokelewa kwa mikono miwili na mashabiki zinakuja miezi takriban miezi 11 tangu Ali Kiba achangamshe Bongo Fleva na albamu yake ya kuitwa "Only One King" ambayo ilisheheni ngoma tofauti tofauti kama ikiwemo Utu na Bwana Mdogo.

Tile ni ngoma ambayo Ali Kiba anatumia ladha ya muziki wa kikongo kuelezea namna ambavyo anamkumbuka mpenzi wake wa zamani ambapo kupitia kibao hiki Ali Kiba anaonesha ni kwa jinsi gani amekuwa akiteseka tangu alipoachana na mwandani wake.  

https://www.youtube.com/watch?v=miGzPizbDFw

Asali ni ngoma halisi yenye vionjo vya Baibuda na Bongo Fleva, ambapo Ali Kiba anazungumzia namna gani ambavyo mapenzi anayopata kutoka kwa mpenzi wake ni matamu kama, vile asali. Ngoma ya Asali imetayarishwa na Mocco Genius kutoka Tanzania ambaye pia alishiriki kuandaa ngoma ya Zuchu ya kuitwa "Cheche".

Kufikia sasa ngoma hizi mbili yaani Asali na Tile hazina video, ila video za ngoma, hizi mbili zinatarajiwa kuwafikia mashabiki hivi karibuni. Aidha ngoma hizi zonatarajiwa kusindikiza vyema ziara ya kimuziki ya Ali Kiba nchini Marekani ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=2bwe9cXvTHs

 

 

Leave your comment