KFC Wakanusha Kuchukua Hatua Za Kisheria Dhidi Ya Kylian Mbappe
23 September 2022
[Picha: sportbible.com]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Kampuni ya vyakula vya haraka ya KFC imekanusha kutaka kuchukua hatua za kisheria kwa shirikisho la soka la nchini Ufaransa baada ya Alain Beral Makamu wa Rais wa KFC nchini ufaransa kuja na tishio hilo. Habari hii imekuja mara baada ya Kylian Mbappe mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa kugoma kupiga picha za matangazo kwa kile walichosema ni Hatimiliki ya picha za nyota huyo wa soka.
Tamko hilo la Alain Beral limekanushwa na kampuni hiyo na kusema kuwa hayo ni maneno binafsi ya Bwana Beral na pia taratibu za kusuluhisha jambo hilo zitafuatwa kwa kuangalia pande zote zenye malalamilo na mlalamikiwa .
Licha ya KFC kujiweka mbali na maneno ya bwana Beral pia mwanasheria wa mshambuliaji huyo wa timu ya Paris Saint Germain Bibi Deiphine Verheyden kusema kazi yake ni kumsikiliza mteja wake na kumsaidia kuchambua mambo yenye utata.
Mara baada ya Sakata hilo kutokea Timu ya Taifa ya Ufarana imesema itatoa muongozo mpya juu ya kuboresha hatimiliki za matangazo Pamoja na sheria za matangazo baada ya Mbappe kutoa pingamizi kwa wadhamini hao.
Wakati shirikisho wa soka la nchini Ufaransa kuendelea na kutafuta suluhisho juu ya jambo hili ikumbukwe kuwa KFC ndio wadhamini wakuu wa soka la nchini Ufaransa na pia mechi za hivi karibuni Ufaransa watakuta na Austria na baadaye Denmark katika mechi za kimataifa.
Leave your comment