Lyrics: Harmonize - Nitaubeba

[Picha: Youtube]

Bonyeza Hapa kusubscribe na Kupakua DJ Mixes Maalum

Imagine uko jangwani umepotea mchana juani unatembea

Utokapo ni mbali uendapo ni mbali

Mara ngamia mbebaji akatokea na kukushusha mzigo uliokuelemea

Upate afadhali pole na safari

And that's why today to me yote tisa ila kumi umeonesha maana ya upendo

Si kwa maneno bali kwa vitendo,

Umeridhika na nilichonacho vya watu hutoleagi macho

Siku nikiwa sina twalala Oooh baby twalala

Aaaah baby if i close my eyes mi namuomba Mungu akulinde

Na akusimamie we ndo pacha wangu mie

Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena, sikusikii ukilia sikusikii ukisema

Niko busy na boo jamani nimeshasema, niko busy na baby na msalaba wake

Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba na ntafika nao kiume

Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha) nitaubeba (ama kwenye shibe na njaa)

La kwako ndo langu my darling na ntafika nao kiume

Imagine hujifahamu umezimia umewekewa damu zinaingia

Bomba ikafunguka na huwezi hata nyanyuka

Mara dakitari wa zamu akaingia umepata fahamu unamwangalia

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Machozi yanakuanguka unatamani funguka

And that’s why today to me yote tisa ila kumi unanifurahisha kwenye tendo

Au unipe penzi la magendo

Aaaah baby if i close my eyes mi namuomba Mungu akulinde

Na akusimamie we ndo pacha wangu mie

Eti siku hizi vipi mbona sikusikii tena, sikusikii ukilia sikusikii ukisema

Niko busy na boo jamani nimeshasema, niko busy na baby na msalaba wake

Nitaubeba, nitaubeba nitaubeba na ntafika nao kiume

Nitaubeba (iwe kwenye shida na raha) ntaubeba (ama kwenye shibe na njaa)

La kwako ndo langu my darling na ntafika nao kiume

Iwe kwenye shida na raha ama kwenye shibe na njaa

La kwako ndo langu my darling

https://www.youtube.com/watch?v=ctZSzhBURiY

Leave your comment