Uchambuzi Mechi Ya Manchester City Vs Borrussia Dortmund

[Picha: skysports.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Katika usiku wa Mabingwa Ulaya, Manchester City wameshinda magoli 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund. Ushindi huo unawafanya City waongoze katika kundi G baada ya Mzunguko wa pili wa Ligi hiyo katika mechi iliyochezwa uwanja wa Etihad.

Dortmund walitangulia kupata goli la kwanza kupitia kwa Jude Bellingham baada ya Marco Reus kumpatia pasi iliyopelekea goli hilo katika dakika ya 56 ya kipindi Cha pili cha mchezo huo.

Katika dakika ya 80 ya mchezo huo John stone akiwa nje kabisa ya boksi anafanikiwa kusawazisha bao hilo baada ya De Bruyne kumsogezea mpira na kuuweka kambani.

Baada ya dakika nne kupita tangu goli la kusawazishwa, straika wa Manchester City Erling Braut Haaland anafanikiwa kuweka bao la pili kambani baada ya Joao Cancelo kumpatia pasi ya usaidizi wa goli na mfungaji huyo kupita katikati ya walinzi wa Dortmund na kuingia kambani.

Get Free Music Updates and Mixes on Telegram

City chini ya Guardiola wameweza kuongoza katika umiliki wa mpira kwa asilimia 66 huku wao Borrussia wakiwa na asilimia 34.

Vijana wa Pep Guardiola wao hawakuwa na maoteo yoyote lakini kwa upande wa kikosi Cha Edin Terzic wao walipata oteo moja. Kona City walikuwa nazo sita huko Dortmund wakiwa na Kona mbili.

Wakati wa mchezo huo ukiwa unaendelea mashuti ya moja kwa moja katika lango la Dortmund yalikuwa 3 kwa City na wapinzani wao wakipata mashuti 2.

Dortmund walipata kadi 3 za njano na City wakiwa na kadi 3 za njano. Katika kadi hizo tatu za City moja ilikuwa ya Kocha wao Josep Guardiola. Hakuna kadi nyekundu katika mchezo huo.

Manchester City pamoja na Borrussia Dortmund ni timu mbili zinazotarajiwa kumaliza kama vinara katika kundi G la Ligi ya mabingwa Ulaya.

Leave your comment