Wasanii 5 Kutoka Tanzania Walioshinda Tuzo Kubwa Za Kimataifa
14 September 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Ukweli ni kuwa kwa muziki wa Tanzania ulipofikia, Bongo Fleva imekuwa tena sio tu bidhaa ya Tanzania au Afrika Mashariki bali imeweza kupenya katika mataifa mbalimbali na ndio maana wasanii wa kitanzania wameweza kujishindia tuzo mbalimbali zenye hadhi kubwa duniani.
Wafuatao ni wasanii watano kutoka Tanzania ambao wameshinda tuzo kubwa za kimataifa :
Ali Kiba
Ali Kiba alipeperusha vyema bendera ya Tanzania mwaka 2016 baada ya kushinda tuzo ya MTV EMA kama msanii bora kutokea Afrika, tuzo ambayo mara ya kwanza alipokea Wizkid lakini baada ya muda waandaaji walikiri kukosea, kisha kumpatia tuzo hiyo Ali Kiba.
Kando na MTV EMA pia Ali Kiba amebeba tuzo nyingine za kimataifa ikiwemo Soundcity kupitia video yake ya "Aje", Afrimma pamoja na tuzo za NAFCA
Nandy
Mwaka 2017 Nandy alijihakikishia nafasi za juu kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kushinda tuzo ya AFRIMA kama msanii wa bora kike kutokea Afrika huku akiwashinda wasanii kama Tiwa Savage, Sho Madjozi pamona na Aya Nakamura kwenye kipengele hicho.
Tuzo nyingine kubwa za kimataifa ambazo Nandy ameshinda ni pamoja na tuzo za AMI kama msanii bora chipukizi mwaka 2018 pamoja na AEUSA ambapo mwaka 2021 alishinda kama msanii bora wa Afrika Mashariki.
Diamond Platnumz
Tangu aanze muziki Diamond Platnumz ameshinda tuzo zaidi ya 70 mojawapo ikiwa ni tuzo ya MTV MAMA zinazoandaliwa na kituo cha MTV Base ambapo kwa mwaka 2015 alikuwa ni mtanzania wa kwanza kushinda kipengele cha Mtumbuizaji bora wa mwaka kwenye tuzo hizo.
Kando na tuzo hiyo Diamond Platnumz pia ameshinda tuzo za Afrimma, Soundcity, Headies na nyinginezo nyingi.
Rayvanny
Mwaka 2017 Rayvanny aliweka rekodi ya kuwa MwanaAfrika mashariki wa pili na Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo ya BET ambapo alishinda tuzo ya Best International Viewers Choice Awards akiwashinda wasanii wakubwa ikiwemo Falz kutokea nchini Nigeria.
Rayvanny pia ametajwa kuwania tuzo ya msanii bora chipukizi kwa mwaka 2017 kwenye tuzo za AFRIMA pamoja na MTV MAMA.
Vanessa Mdee
Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka mzuri sana kwa Vanessa Mdee kwani aliweza kushinda tuzo ya AFRIMA kama msanii bora wa Afrika Mashariki pamoja na Afrimma kama msanii wa Pop kupitia ngom yake ya Hawajui.
Leave your comment