Uchambuzi mechi ya Zalan Fc Vs Yanga FC

[Picha: Wasomoajira.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mabingwa wa ligi kuu ya NBC nchini Tanzania Young African Sc siku ya Jumamosi waliweza kuwakabili Zalan Fc Rumbek kwa ushindi wa bao 4-0. Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam. Katika mchezo huo Fiston Mayele aliweza kuwaka kambani jumla ya magoli matatu na huku Feisal Salum akiweka kambani bao lake la kwanza katika ligi hiyo ya Mabingwa Afrika.

Ukiwa ni mzunguko wa kwanza wa awali Yanga waliweza kuutawala mpira kwa 80%  katika kipindi cha kwanza licha ya kipindi hicho kuisha bila ya kupata matokeo. Zalan Fc walijikuta wakicheza nusu uwanja na mashambulizi kuwa makali kutokea upande wa Yanga licha ya kujitahidi na kulinda lango lao katika kipindi hicho cha kwanza.

Get Free Music Updates and Mixes on Telegram

Kwa ujumla katika mchezo huo Yanga ndio walibeba nafasi kubwa ya ushindi. 85% ya mchezo ilitawaliwa na mimba hiyo ya Jangwani huku Zalan wao wakitawala mpira kwa asilimia 15% pekee. Kwa upande wa kona Zalan Fc walipata kona moja huku wao Yanga wakiwa na jumla ya kona 5. Kwa umiliki wa Yanga katika mchezo huo walipata mashuti takribani 14 ya moja kwa moja katika lango la Zalan huku wapinzani wao hao wakiwa na shuti moja pekee katika lango la Yanga.

Kwa upande wa suala la maoteo Zalani walikuwa na maoteo mawili na Yanga wao wakiwa na maoteo nane ambayo maoteo mawili yaliingia katika lango la Zalan Fc. Kadi zilizotelewa katika mchezo huo ni kadi moja ya njano kwa mchezaji kutokea Zalan na hakuna kadi nyekundu.

Kutokana na suala a ubovu wa miundombinu ya viwanja vya michezo nchini Sudan Kusini, Yanga wamelazimika kupata faida ya kuwa wenyeji wa mechi zote mbili za nyumbani na ugenini watakazoshiriki na Zalan Fc. Hivyo basi katika mechi hii Zalan wamehesabika kuwa katika uwanja wao wa nyumbani kutokana na viwanja vya nchini kwao kutokukidhi viwango vya FIFA.

Timu ya Zalan Fc hii imekuwa mara yake ya kwanza kushiriki mashindano hayo mkubwa ya Afrika tangu Sudan Kusini ilipopata uhuru wake mwaka 2011, na katika ligi kuu ya Sudan kusini katika msimu uliopita timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya pili.

Leave your comment