Uchambuzi Mechi Ya Nyasa Big Bullets Vs Simba Sc
12 September 2022
[Picha: assengaonline.com]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Timu ya Nyasa big bullets ya nchini Malawi imeambulia kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Wekundu wa Msimbazi Smba ya nchini Tanzania. Mchezo huo ulichezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa wa Bingu na Nyasa wao wakiwa ndio wenyeji wa mchezo huo katika mkondo wa kwanza katika mzunguko wa awali katika ligi ya mabingwa Africa.
Simba walianza kuziona nyavu za wenyeji wao hao katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza cha mchezo. Goli hilo liliwekwa kambani na Moses Phiri baada ya kupiga sarakasi (Acrobatics) na kuwacha mabeki wa timu pinzani wakishangaa mpira ukizama kambani.
Get Free Music Updates and Mixes on Telegram
Goli la pili lilifungwa na Captain John Raphael Bocco katika dakika ya 80 ya kipindi cha pili cha mchezo baada ya kuipokea pasi kutoka kwa Clatous Chama. Bao hii likawaweka Simba kifua mbele katika mzunguko huo wa kwanza na sasa wanasubiri mechi ya marudiano Jumamosi hii
Wakati wa mchezo ukiwa unendelea katika dimba hilo la Bingu, Nyasa walipata kona nne nyuma ya Simba ambao wao walikuwa na kona tatu. Kwa upande wa suala la nidhamu mchezo huo ulitawaliwa na nidhamu ya hali ya juu baada ya dakika 90 kuisha bila ya kadi yoyote kutolewa.
Goli la kwanza kutoka kwa Simba limeweza kujizolea umaarufu, na hii ni kutoka goli hilo kutotofautiana sana na goli alilofunga Pape Osman Sahko ambalo liilompa ushindi wa tuzo za CAF raia huyo kutokea Senegal kama goli bora la mwaka kwa msimu wa mwaka 2021-2022.
Leave your comment