Nyimbo Mpya: Rosa Ree 'Threesome', 'Tell Me' Beka Flavor na Nyimbo Nyingine Mpya Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwezi Septemba umeendelea kunoga na hii ni kutokana na mashabiki kuendelea kupokea dozi nzito ya burudani kutoka kwa wasanii wa Tanzania ambao kwa mara nyingine wameendelea kutoa ngoma kali.

Zifuatazo ni ngoma kali mpya kutoka Tanzania Wiki Hii :

Threesome - Rosa Ree Ft. Chemical & Frida Amani (Official Video)

Hii ni kazi mpya ya wasanii watatu wa kike ambao wanaangazia ubabe wao kama wasanii wa hip hop ndani ya wimbo huu. Rosa Ree, Chemical na Frida Amani wameua humu ndani na heshima zao sasa zaendelea kupanda zaidi.

https://www.youtube.com/watch?v=pPVJ9BWatuA

Tell Me - Beka Flavour.

Mwanamuziki Beka Fleva alitetemesha Bongo Fleva wiki hii na ngoma yake ya kuitwa "Tell Me" ambayo ndani yake anamuomba mpenzi wake aweze kumueleza ni wapi amekosea. Huu ni mwendelezo wa Beka Flavour kuendelea kutoa ngoma kali kwa mashabiki zake.

https://www.youtube.com/watch?v=TF0AATPWeG8

Read Again - Moni Centrozone Ft G Nako

Wiki hii Moni Centrozone aliweza kuheshimisha muziki wa Hip Hop kwa kuachia "Read Again" ngoma ambayo ndani yake ameweza kutoa mafunzo na mawazo yake kuhusu maisha. Ngoma hii imetayarishwa na Baddest 47 huku maandalizi ya mwisho yakishughulikiwa na Mr T Touch.

https://www.youtube.com/watch?v=pPXntD31Nxw

Singeli Twista - Sholo Mwamba Ft AY Masta

Hii ni moja ya ngoma ambayo ilisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki na bila shaka Sholo Mwamba na AY kuleta kilichotarajiwa kwenye ngoma hii ya songeli ambayo muda mfupi tu tangu kuachiwa kwake imekuwa ni ngoma pendwa baina ya mashabiki sio tu wa Singeli bali mashabiki wa Hip Hop kwa ujumla

https://www.youtube.com/watch?v=Ua4PHA6tbEU

Leo - Mabantu Ft Marioo

Kwa mara nyingine tena kundi la Mabantu linakutana na Marioo kwenye wimbo wa kuitwa Leo ambao ndani yake wasanii hawa wanamshukuru Mungu kwa kuweza kuwafanyia mambo makubwa katika maisha yao. Kufuatia mashahiri mazuri na mdundo wa kuvutia, wengi wamepokea vyema ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=IPdEwqR1ECg

Mzuri - Barnaba Classic Ft Rayvanny

Baada ya Hadithi, Barnaba Classic ameachia video ya Mzuri, video ambayo ukiweka kando ubora wa picha pia mandhari na wahusika wake wamefanya video hiyo ambayo imeongozwa na Eris Mzava kuwa ya kipekee sana.

https://www.youtube.com/watch?v=xJz52_GmVYc

 

Leave your comment