Nyimbo Bora Baina Ya Wasanii Wa Singeli Na Bongo Fleva

[Picha: Screengrab/YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Ukweli ni kuwa muziki wa singeli umeendelea kunawiri nchini Tanzania hasa katika miaka ya hivi karibuni. Moja ya vitu ambavyo vimechagiza ukuaji wa singeli ushirikiano wa kisanaa baina ya wanamuziki wa singeli na wasanii wa Bongo Fleva ambao kwa miaka ya hivi karibuni wameonekana kupenda na kuupokea kwa mikono miwili muziki wa singeli.

Zifuatazo ni collabo tano bora baina ya wasanii wa Bongo Fleva na wasani wa Singeli:

Wanga - Meja Kunta Ft Lavalava

Wanga ni wimbo bao ulimhusisha Meja Kunta na msanii wa WCB wa kuitwa Lavalava ambaye bila shaka aliweza kuifanyia haki ngoma hii ambayo iliweza kumtambulisha vyema Meja Kunta kwa mashabiki. Ngoma hii imeweza kufanya vizuri sana huko Youtube na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 6 huko Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=SV1ra6fchW0

Do Lemi Go - Kinata MC Ft Ibraah

Do Lemi Go itaendelea kusimama kama moja ya ngoma za kibunifu zaidi kwenye muziki wa singeli na hii ni kutokana na ufundi wa Kinata MC kukopa baadhi ya maneno ya kiingereza na kuyaweka kwenye kwenye ngoma hii, ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kwa msanii wa singeli kufanya hivyo. Video kali na mdundo wa kusisimua umechagiza ngoma hii kutazamwa mara Milioni 2.3 kwenye mtandao wa YouTube

https://www.youtube.com/watch?v=VubqA0ej12w

Ex Wangu Remix - Hamissa Mobetto Ft Seneta Kilaka

Ukiweka kando mashahiri mepesi ya Hamisa Mobetto katika ngoma hii pamoja na muingiliano mzuri wa sauti baina ya wasanii hawa, video kali ambayo bila shaka iliteka hisia za wapenda singeli wengi nchini Tanzania, ilichangia ngoma hiii kufanya vizuri.

Ngoma hii iliweka rekodi ya kuwa moja ya ngoma za singeli zilizotazamwa zaidi Youtube kwa mwaka 2021.

https://www.youtube.com/watch?v=CmSgffQYaSo

Miss Buza - Rayvanny Ft Dullah Makabila

Rayvanny aliweza kutikisa singeli na ngoma yake ya Miss Buza ambayo alimshirikisha Dulla Makabila. Kupitia ngoma hii, Rayvanny aliweza kuchanganya muziki wa Bongo Fleva na singeli kutengeneza ngoma ya aina yake ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 10 kwenyr mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=0PWCMHTJRn4

Kazi Kazi - Professor Jay Ft Sholo Mwamba

Professor Jay alikuwa ni moja ya wasanii wa kwanza kabisa wa Hip Hop kuuamini na kuupenda muziki wa singeli, upendo uliopelekea miaka 6 iliyopita kufanya ngoma ya kuitwa Kazi Kazi akiwa na Sholo Mwamba. Ngoma hii ilikuwa ni moja ya ngoma zilizoleta mapinduzi malubwa kwenye muziki wa singeli nchini.

https://www.youtube.com/watch?v=cPJ_pqmddWk

Leave your comment